Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Hosea 2:23 - Swahili Revised Union Version

23 Nami nitampanda katika nchi kwa ajili yangu mwenyewe; nami nitamrehemu yeye asiyepewa rehema; nami nitawaambia wale wasiokuwa watu wangu, Ninyi ndinyi watu wangu; nao watasema, Wewe ndiwe Mungu wangu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

23 Nitamwotesha Yezreeli katika nchi; nitamhurumia ‘Asiyehurumiwa’, na wale walioitwa ‘Siwangu’, nitawaambia, ‘Nyinyi ni watu wangu.’ Nao watasema, ‘Wewe ni Mungu wetu.’”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

23 Nitamwotesha Yezreeli katika nchi; nitamhurumia ‘Asiyehurumiwa’, na wale walioitwa ‘Siwangu’, nitawaambia, ‘Nyinyi ni watu wangu.’ Nao watasema, ‘Wewe ni Mungu wetu.’”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

23 Nitamwotesha Yezreeli katika nchi; nitamhurumia ‘Asiyehurumiwa’, na wale walioitwa ‘Siwangu’, nitawaambia, ‘Nyinyi ni watu wangu.’ Nao watasema, ‘Wewe ni Mungu wetu.’”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

23 Nitampanda katika nchi kwa ajili yangu mwenyewe; nami nitaonesha pendo langu kwake yule ambaye nilimwita, ‘Si Mpendwa Wangu.’ Nitawaambia wale walioitwa, ‘Sio Watu Wangu,’ ‘Ninyi ni Watu Wangu’; nao watasema, ‘Wewe ndiwe Mungu wangu’.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

23 Nitampanda katika nchi kwa ajili yangu mwenyewe; nami nitaonyesha pendo langu kwake yule ambaye nilimwita, ‘Si mpenzi wangu.’ Nitawaambia wale walioitwa, ‘Sio watu wangu,’ ‘Ninyi ni watu wangu’; nao watasema, ‘Wewe ndiwe Mungu wangu.’ ”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

23 Nami nitampanda katika nchi kwa ajili yangu mwenyewe; nami nitamrehemu yeye asiyepewa rehema; nami nitawaambia wale wasiokuwa watu wangu, Ninyi ndinyi watu wangu; nao watasema, Wewe ndiwe Mungu wangu.

Tazama sura Nakili




Hosea 2:23
33 Marejeleo ya Msalaba  

Ndiwe Mungu wangu, nami nitakushukuru, Ndiwe Mungu wangu, nami nitakutukuza.


Miisho yote ya dunia itakumbuka, Na watu watamrejea BWANA; Jamaa zote za mataifa watamsujudia.


Masheki watakuja kutoka Misri, Kushi itahimiza kumnyoshea Mungu mikono yake.


Na uwepo wingi wa nafaka Katika ardhi juu ya milima; Matunda yake na yawayewaye kama ilivyo katika milima ya Lebanoni, Na watu wa mjini wasitawi kama majani ya nchi.


Mpendwa wangu ni wangu, na mimi ni wake; Hulisha kundi lake penye nyinyoro.


Mmoja atasema, Mimi ni wa BWANA; na mwingine atajiita kwa jina la Yakobo; na mwingine ataandika juu ya mkono wake, Kwa BWANA, na kujiita kwa jina la Israeli.


Ee BWANA, nguvu zangu, ngome yangu, na kimbilio langu siku ya taabu, kwako wewe watakuja mataifa yote toka ncha za dunia, wakisema, Baba zenu hawakurithi kitu ila uongo, naam, ubatili na vitu visivyofaa.


Nanyi mtakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu.


Tazama, siku zinakuja, asema BWANA, nitakapoipanda nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda, mbegu ya mwanadamu na mbegu ya mnyama.


nao watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao;


ndipo nitawatupilia mbali wazao wa Yakobo, na Daudi, mtumishi wangu, hata nisitwae wazao wake watawale juu ya wazao wa Abrahamu, na Isaka, na Yakobo; kwa maana nitawarudisha wafungwa wao, nami nitawarehemu.


Nami nitawaokoeni kutoka kwa uchafu wenu wote; nitaiamuru ngano iongezeke, wala sitawaletea njaa tena.


Akachukua mimba tena, akazaa mtoto wa kike, BWANA akamwambia, Mwite jina lake Lo-ruhama; kwa maana sitairehemu nyumba ya Israeli tena, nisije nikawasamehe kwa njia yoyote.


Watanililia, Mungu wangu, sisi Israeli tunakujua.


Nami nitawapanda kama mbegu kati ya mataifa; nao watanikumbuka katika nchi zilizo mbali; nao watakaa pamoja na watoto wao; tena watarudi.


Nami nitalileta fungu lile la tatu na kulipitisha kati ya moto, nami nitawasafisha kama fedha isafishwavyo, nami nitawajaribu kama dhahabu ijaribiwavyo; wataliitia jina langu, nami nitawasikia; mimi nitasema, Watu hawa ndio wangu; nao watasema, BWANA ndiye Mungu wangu.


Hata itakuwa, ya kwamba kila mtu aliyesalia wa mataifa yote, waliokuja kupigana na Yerusalemu, atakwea mwaka baada ya mwaka ili kumwabudu Mfalme, BWANA wa majeshi, na kuiadhimisha sikukuu ya Vibanda.


Naye BWANA atakuwa Mfalme wa nchi yote; siku hiyo BWANA atakuwa mmoja, na jina lake moja.


Na mataifa mengi watajiunga na BWANA katika siku ile, nao watakuwa watu wangu; nami nitakaa kati yako, nawe utajua ya kuwa BWANA wa majeshi amenituma kwako.


Kwa maana tokea maawio ya jua hata machweo yake jina langu ni kuu katika mataifa; na katika kila mahali unatolewa uvumba na dhabihu safi kwa jina langu; maana jina langu ni kuu katika mataifa, asema BWANA wa majeshi.


Au je! Mungu ni Mungu wa Wayahudi tu? Siye Mungu wa Mataifa pia? Naam, ni Mungu wa Mataifa pia;


Yakobo, mtumwa wa Mungu, na wa Bwana Yesu Kristo, kwa makabila kumi na mawili waliotawanyika; salamu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo