Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Hesabu 7:10 - Swahili Revised Union Version

10 Kisha wale wakuu wakatoa matoleo kwa ajili ya kuiweka wakfu madhabahu, katika siku hiyo iliyotiwa mafuta, wakuu wakayatoa matoleo yao mbele ya madhabahu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Viongozi hao wakatoa sadaka kwa ajili ya kuiweka wakfu madhabahu siku ile ilipopakwa mafuta; walitoa sadaka zao mbele ya madhabahu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Viongozi hao wakatoa sadaka kwa ajili ya kuiweka wakfu madhabahu siku ile ilipopakwa mafuta; walitoa sadaka zao mbele ya madhabahu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Viongozi hao wakatoa sadaka kwa ajili ya kuiweka wakfu madhabahu siku ile ilipopakwa mafuta; walitoa sadaka zao mbele ya madhabahu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Madhabahu yalipopakwa mafuta, viongozi walileta sadaka zao kwa ajili ya kule kuwekwa wakfu kwake na kuziweka mbele ya madhabahu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Wakati madhabahu yalitiwa mafuta, viongozi walileta sadaka zao kwa ajili ya kule kuwekwa wakfu kwake na kuziweka mbele ya madhabahu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

10 Kisha wale wakuu wakatoa matoleo kwa ajili ya kuiweka wakfu madhabahu, katika siku hiyo iliyotiwa mafuta, wakuu wakayatoa matoleo yao mbele ya madhabahu.

Tazama sura Nakili




Hesabu 7:10
12 Marejeleo ya Msalaba  

Sulemani akatoa sadaka za amani, alizomtolea BWANA, ng'ombe elfu ishirini na mbili, na kondoo elfu mia moja na ishirini. Ndivyo mfalme na wana wa Israeli wote walivyoiweka wakfu nyumba ya BWANA.


Mfalme Sulemani akatoa sadaka ya ng'ombe elfu ishirini na mbili, na kondoo elfu mia moja na ishirini. Ndivyo mfalme na watu wote walivyoifanya wakfu nyumba ya Mungu.


Siku ya nane wakaita kusanyiko la makini; kwa maana waliadhimisha kuitakasa madhabahu siku saba, na sikukuu siku saba.


Basi, walipouweka wakfu ukuta wa Yerusalemu wakawatafuta Walawi katika mahali pao pote, ili kuwaleta Yerusalemu, ili waweze kusherehekea kuweka wakfu pamoja na furaha, na kwa shukrani, na kwa kuimba, kwa matoazi, vinanda na vinubi.


Wakatoa dhabihu nyingi siku ile, wakafurahi; kwa kuwa Mungu amewafurahisha furaha kuu; na wanawake pia na watoto wakafurahi; hata ikasikika mbali sana furaha hiyo ya Yerusalemu.


Ee BWANA, nitakutukuza kwa maana umeniinua, Wala hukuwafurahisha adui zangu juu yangu.


Ilikuwa siku hiyo Musa alipokwisha kuisimamisha maskani, na kuitia mafuta, na kuitakasa, na vyombo vyake vyote, na hiyo madhabahu na vyombo vyake vyote, na kuvitia mafuta, na kuvitakasa;


Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, Watasongeza matoleo yao, kila mkuu kwa siku yake, kwa ajili ya kuiweka wakfu madhabahu.


Hayo ndiyo matoleo yaliyotolewa na wakuu wa Israeli kwa ajili ya kuiweka wakfu madhabahu, siku hiyo ilipotiwa mafuta; sahani za fedha kumi na mbili, na bakuli za fedha kumi na mbili, na vijiko vya dhahabu kumi na viwili;


na ng'ombe wote waliokuwa wa dhabihu ya sadaka za amani ni ng'ombe dume ishirini na wanne, na hao kondoo dume walikuwa ni sitini, na hao mbuzi dume walikuwa ni sitini, na wana-kondoo dume wa mwaka mmoja walikuwa sitini. Hayo ndiyo matoleo yaliyotolewa kwa ajili ya kuiweka wakfu madhabahu, baada ya hiyo madhabahu kutiwa mafuta.


Na maofisa na waseme na watu, na kuwaambia, Ni mtu gani aliye hapa aliyejenga nyumba mpya, wala hajaiweka wakfu? Aende akarudi nyumbani kwake, asije akafa mapiganoni, ikawekwa wakfu na mtu mwingine.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo