Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Hesabu 6:2 - Swahili Revised Union Version

2 Nena na watu wa Israeli, uwaambie, Mwanamume au mwanamke atakapoweka nadhiri maalumu, nadhiri ya Mnadhiri, ili ajiweke wakfu kwa BWANA;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 “Wape Waisraeli maagizo yafuatayo: Iwapo mwanamume au mwanamke ataweka nadhiri maalumu, nadhiri ya kujiweka wakfu, akajitenga kwa ajili ya Mwenyezi-Mungu,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 “Wape Waisraeli maagizo yafuatayo: Iwapo mwanamume au mwanamke ataweka nadhiri maalumu, nadhiri ya kujiweka wakfu, akajitenga kwa ajili ya Mwenyezi-Mungu,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 “Wape Waisraeli maagizo yafuatayo: Iwapo mwanamume au mwanamke ataweka nadhiri maalumu, nadhiri ya kujiweka wakfu, akajitenga kwa ajili ya Mwenyezi-Mungu,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 “Sema na Waisraeli na uwaambie: ‘Ikiwa mwanaume au mwanamke anataka kuweka nadhiri maalum, nadhiri ya kutengwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kama Mnadhiri,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 “Sema na Waisraeli na uwaambie: ‘Ikiwa mwanaume au mwanamke anataka kuweka nadhiri maalum, nadhiri ya kutengwa kwa ajili ya bwana kama Mnadhiri,

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

2 Nena na watu wa Israeli, uwaambie, Mwanamume au mwanamke atakapoweka nadhiri maalumu, nadhiri ya Mnadhiri, ili ajiweke wakfu kwa BWANA;

Tazama sura Nakili




Hesabu 6:2
21 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana itajulikanaje kuwa nimepata neema mbele zako, mimi na watu wako? Siyo kwa sababu unakwenda pamoja nasi, hata mimi na watu wako tutengwe na watu wote walio juu ya uso wa nchi?


Ajitengaye na wenzake hutafuta matakwa yake mwenyewe; Hushindana na kila shauri jema.


Lakini wakasema, Hatutakunywa divai; kwa maana Yonadabu, mwana wa Rekabu, baba yetu, alituamuru, akisema, Msinywe divai, ninyi wala wana wenu, hata milele;


Nanyi mtakuwa watakatifu kwangu; kwa kuwa mimi BWANA ni mtakatifu nami nimewatenga ninyi na mataifa, ili kwamba muwe wangu.


Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Hapo mtu atakapoondoa nadhiri, hizo nafsi za watu zitakuwa kwa BWANA, kama utakavyowahesabia wewe.


Tena mwanamke atakapomwekea BWANA nadhiri, na kufunga nafsi yake kwa kifungo, naye aishi katika nyumba ya babaye, katika ujana wake;


Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia,


Kwa sababu atakuwa mkuu mbele za Bwana; hatakunywa divai wala kileo; naye atajazwa Roho Mtakatifu hata tangu tumboni mwa mamaye.


Baada ya hayo Paulo akazidi kukaa huko siku nyingi, kisha akaagana na ndugu akaabiri kwenda Shamu; na Priskila na Akila wakaenda pamoja naye, alipokwisha kunyoa kichwa chake huko Kenkrea; maana alikuwa ana nadhiri.


Paulo, mtumwa wa Kristo Yesu, aliyeitwa kuwa mtume, na kutengwa aihubiri Injili ya Mungu;


Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.


Lakini Mungu, aliyenitenga tangu tumboni mwa mama yangu, akaniita kwa neema yake,


ambaye hana haja kila siku, mfano wa wale makuhani wakuu wengine, kwanza kutoa dhabihu kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe, kisha kwa ajili ya dhambi za hao watu; maana yeye alifanya hivi mara moja, alipojitoa nafsi yake.


Asile kitu chochote kitokacho katika mzabibu, wala asinywe divai, wala mvinyo, wala asile kitu chochote kilicho najisi; hayo yote niliyomwamuru na ayatunze.


Basi sasa, jihadhari, nakuomba, usinywe divai wala kileo, wala usile kitu kilicho najisi;


kwani tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume; na wembe usipite juu ya kichwa chake; maana mtoto huyo atakuwa mnadhiri wa Mungu tangu tumboni; naye ataanza kuwaokoa Israeli na mikono ya Wafilisti.


Ndipo alipomwambia yote yaliyokuwa moyoni mwake, akamwambia, Wembe haukupita juu ya kichwa changu kamwe; maana mimi nimekuwa Mnadhiri wa Mungu, tangu tumboni mwa mama yangu; nikinyolewa, ndipo nguvu zangu zitanitoka, nami nitakuwa dhaifu, nitakuwa kama wanadamu wenzangu.


kwa sababu hiyo mimi nami nimempa BWANA mtoto huyu; wakati wote atakaokuwa hai amepewa BWANA. Naye akamwabudu BWANA huko.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo