Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Hesabu 4:12 - Swahili Revised Union Version

12 kisha watavitwaa vile vyombo vyote vya utumishi wavitumiavyo katika mahali patakatifu, na kuvitia katika nguo ya rangi ya samawati, na kuvifunika kwa ngozi za pomboo, na kuvitia juu ya miti ya kuvichukulia.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Watavichukua vyombo vyote vinavyotumika mahali patakatifu, watavifunga kwa kitambaa cha buluu na kuvifunika kwa ngozi laini ya mbuzi, kisha wataviweka juu ya mipiko yake ya kuchukulia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Watavichukua vyombo vyote vinavyotumika mahali patakatifu, watavifunga kwa kitambaa cha buluu na kuvifunika kwa ngozi laini ya mbuzi, kisha wataviweka juu ya mipiko yake ya kuchukulia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Watavichukua vyombo vyote vinavyotumika mahali patakatifu, watavifunga kwa kitambaa cha buluu na kuvifunika kwa ngozi laini ya mbuzi, kisha wataviweka juu ya mipiko yake ya kuchukulia.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 “Watavichukua vyombo vyote vinavyotumika kuhudumia mahali patakatifu, watavisokotea kwenye kitambaa cha buluu na kufunika kwa ngozi za pomboo, na kuviweka juu ya miti ya kuchukulia.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 “Watavichukua vyombo vyote vinavyotumika kuhudumia mahali patakatifu, watavisokotea kwenye kitambaa cha buluu na kufunika kwa ngozi za pomboo, na kuviweka juu ya miti ya kuchukulia.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

12 kisha watavitwaa vile vyombo vyote vya utumishi wavitumiavyo katika mahali patakatifu, na kuvitia katika nguo ya rangi ya samawati, na kuvifunika kwa ngozi za pomboo, na kuvitia juu ya miti ya kuvichukulia.

Tazama sura Nakili

Hesabu 4:12
16 Marejeleo ya Msalaba  

Na baadhi yao walivilinda vyombo vya huduma; kwani huingizwa kwa hesabu, na kutolewa kwa hesabu vile vile.

Na baadhi yao waliwajibika kuviangalia vyombo vya nyumbani, na vyombo vyote vya Patakatifu; pamoja na unga safi, na divai, na mafuta, na ubani, na manukato.

Na Huramu akatengeneza vyungu, sepetu, na mabeseni. Basi Huramu akamaliza kufanya hiyo kazi, aliyomfanyia mfalme Sulemani ya nyumba ya Mungu;

Vyungu, pia sepetu, nyuma na vyombo vingine vyote, Huram-abi akamtengenezea mfalme Sulemani kwa ajili ya nyumba ya BWANA, vilikuwa vya shaba iliyong'arishwa.

Basi Sulemani akavifanya vyombo vyote vilivyokuwamo nyumbani mwa Mungu, madhabahu ya dhahabu pia, nazo meza, ambazo juu yake iliwekwa mikate ya wonyesho;

na mikasi, na mabakuli, na miiko, na vyetezo, vya dhahabu iliyosafika; na kwa habari za mahali pa kuingia nyumbani, milango yake ya ndani ya patakatifu pa patakatifu, na milango ya nyumba, yaani ya hekalu, ilikuwa ya dhahabu.

na ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu, na ngozi za pomboo, na miti ya mjohoro,

Sawasawa na haya yote nikuoneshayo, mfano wa maskani, na mfano wa samani zake zote, ndivyo mtakavyovifanya.

na mavazi yenye kufumwa kwa uzuri, na mavazi matakatifu ya Haruni kuhani, na mavazi ya wanawe, ili kutumika kwa ajili ya huduma yao ya ukuhani;

Nao watavitunza vyombo vyote vya hema ya kukutania, na kuwatumikia wana wa Israeli, kwa kuhudumu katika maskani.

Tena watatandika nguo ya rangi ya samawati juu ya madhabahu ya dhahabu, na kuifunika kwa ngozi za pomboo, na kuitia ile miti yake;

Nao watayaondoa hayo majivu madhabahuni; na kutandika nguo ya rangi ya zambarau juu yake;

kisha ataweka juu yake ngozi laini ya mnyama za kulifunikia, na kutandika juu yake nguo ya rangi ya samawati tupu, kisha watatia hiyo miti yake.

Tena juu ya meza ya mikate ya madhabahuni watatandika nguo ya rangi ya samawati, na kuweka juu yake sahani, na miiko, na mabakuli, na vikombe vya kumiminia; na hiyo mikate ya daima itakuwa juu yake;

Kisha watatwaa nguo ya rangi ya samawati, na kukifunika kinara cha taa ya nuru, na taa zake, na makasi yake, na sahani zake za kuwekea makaa, na vyombo vyake vyote vya mafuta, watumiavyo kwa kazi yake;

Tufuate:

Matangazo

Matangazo