Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Hesabu 35:5 - Swahili Revised Union Version

5 Nanyi mtapima hapo nje ya mji upande wa mashariki dhiraa elfu mbili, na upande wa kusini dhiraa elfu mbili, na upande wa magharibi dhiraa elfu mbili, na upande wa kaskazini dhiraa elfu mbili, huo mji ulio katikati. Hayo ndiyo yatakayokuwa kwao malisho ya miji.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Kwa hiyo, eneo hilo la malisho litakuwa la mita 900, na litaenea kila upande wa mji, mji wenyewe ukiwa katikati. Eneo hilo litakuwa malisho yao kandokando ya miji yao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Kwa hiyo, eneo hilo la malisho litakuwa la mita 900, na litaenea kila upande wa mji, mji wenyewe ukiwa katikati. Eneo hilo litakuwa malisho yao kandokando ya miji yao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Kwa hiyo, eneo hilo la malisho litakuwa la mita 900, na litaenea kila upande wa mji, mji wenyewe ukiwa katikati. Eneo hilo litakuwa malisho yao kandokando ya miji yao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Nje ya mji, pima dhiraa elfu mbili upande wa mashariki, upande wa kusini dhiraa elfu mbili, upande wa magharibi dhiraa elfu mbili, na upande wa kaskazini dhiraa elfu mbili, na mji utakuwa katikati. Eneo hili litakuwa lao la malisho.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Nje ya mji, pima mita 900 upande wa mashariki, upande wa kusini mita 900, upande wa magharibi mita 900, na upande wa kaskazini mita 900, na mji utakuwa katikati. Eneo hili litakuwa lao kwa ajili ya malisho.

Tazama sura Nakili

Hesabu 35:5
3 Marejeleo ya Msalaba  

Na yale malisho ya miji mtakayowapa Walawi, ukubwa wake utakuwa tangu ukuta wa mji kupima kiasi cha dhiraa elfu pande zote.

Na hiyo miji mtakayowapa Walawi, itakuwa miji sita ya kukimbilia, mtakayoweka kwa ajili ya mwenye kumwua mtu, ili akimbilie huko; pamoja na hiyo mtawapa miji arubaini na miwili zaidi.

Na akija Mlawi atokaye katika malango yako mojawapo, katika Israeli yote alipokuwa akikaa, akaja kwa mapenzi yote ya nafsi yake mahali atakapochagua BWANA;

Tufuate:

Matangazo

Matangazo