Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Hesabu 25:4 - Swahili Revised Union Version

4 Kisha BWANA akamwambia Musa, Watwae wakuu wote wa watu hao, uwanyongee juani mbele ya BWANA ili kwamba hizo hasira kali za BWANA ziwaondokee Israeli.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Basi, Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Wachukue viongozi wote wa Israeli, uwanyonge mbele yangu juani, ili ghadhabu yangu dhidi yenu ipite.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Basi, Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Wachukue viongozi wote wa Israeli, uwanyonge mbele yangu juani, ili ghadhabu yangu dhidi yenu ipite.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Basi, Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Wachukue viongozi wote wa Israeli, uwanyonge mbele yangu juani, ili ghadhabu yangu dhidi yenu ipite.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, “Uwachukue viongozi wote wa watu hawa, uwaue hadharani mbele za Mwenyezi Mungu, ili hasira kali ya Mwenyezi Mungu iweze kuondoka kwa Israeli.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 bwana akamwambia Musa, “Uwachukue viongozi wote wa watu hawa, uwaue na uwaweke hadharani mchana peupe mbele za bwana, ili hasira kali ya bwana iweze kuondoka kwa Israeli.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

4 Kisha BWANA akamwambia Musa, Watwae wakuu wote wa watu hao, uwanyongee juani mbele za BWANA ili kwamba hizo hasira kali za BWANA ziwaondokee Israeli.

Tazama sura Nakili




Hesabu 25:4
21 Marejeleo ya Msalaba  

basi, na tutolewe watu saba katika wanawe, nasi tutawatundika mbele za BWANA katika Gibeoni, katika mlima wa BWANA. Mfalme akasema, Nitawatoa.


akawatia mikononi mwa Wagibeoni, nao wakawatundika mlimani mbele za BWANA, nao wakaangamia wote saba pamoja; wakauawa siku za mavuno, za kwanza, mwanzo wa mavuno ya shayiri.


Wakamkasirisha kwa matendo yao; Tauni ikawashambulia.


Musa akawachagua watu wenye uwezo katika Israeli yote, akawaweka wawe vichwa juu ya watu, wakuu wa maelfu, na wakuu wa mamia, na wakuu wa hamsini hamsini, na wakuu wa kumi kumi.


Ni nani ajuaye kwamba Mungu hatageuka na kughairi, na kuiacha hasira yake kali, ili msiangamizwe?


Finehasi, mwana wa Eleazari, mwana wa Haruni kuhani, amezigeuza hasira zangu zisiwe juu ya wana Wa Israeli, kwa kuwa alikuwa na wivu kati yao kwa wivu wangu mimi, hata nisiwaangamize wana wa Israeli katika wivu wangu.


kwa sababu wao wawasumbua ninyi kwa hila zao, ambazo kwa hizo wamewadanganya ninyi katika jambo la Peori, na katika jambo la huyo Kozbi, binti wa mkuu wa Midiani, dada yao, huyo aliyeuawa siku hiyo ya pigo katika jambo la Peori.


Na Israeli wote watasikia na kuogopa, wasifanye tena uovu mfano wa huo katikati yako.


Kumetoka katikati yako mabaradhuli kadha wa kadha, wamewapotoa wenyeji wa mji wao, wakisema, Twendeni tukaabudu miungu mingine msiyoijua;


hakika yako uwapige wenyeji wa mji ule kwa makali ya upanga, kwa kuwaangamiza kabisa, pamoja na vitu vyote vilivyomo, na wanyama walio humo, kwa makali ya upanga.


Kisishikamane na mkono wako kitu chochote katika kitu kilichoharimishwa; ili ageuke BWANA na ukali wa hasira zake akurehemu, akuonee huruma, na kukufanya kuwa wengi, kama alivyowaapia baba zako;


Ikiwa mtu ametenda dhambi ipasayo kufa, akauawa, nawe ukamtundika juu ya mti;


mzoga wake usikae usiku kucha juu ya mti; lazima utamzika siku iyo hiyo; kwani aliyetundikwa amelaaniwa na Mungu; usije ukatia unajisi katika nchi yako akupayo BWANA, Mungu wako, iwe urithi wako.


Macho yenu yameona aliyoyatenda BWANA kwa sababu ya Baal-peori; maana wote waliomfuata Baal-peori, BWANA, Mungu wako, amewaangamiza kutoka kati yako.


Je! Ule uovu wa Peori haututoshi, ambao hamjajitakasa nafsi zenu katika huo hata hivi leo, ijapokuwa ilikuja tauni juu ya mkutano wa BWANA,


Yoshua akawaita Israeli wote, wazee wao, na wakuu wao, na waamuzi wao, na makamanda wao, akawaambia, Mimi ni mzee, nami nimezeeka sana;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo