Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Hesabu 19:13 - Swahili Revised Union Version

13 Mtu yeyote yule agusaye maiti ya mtu aliyekufa, asijitakase, analitia unajisi maskani ya BWANA; na mtu huyo atatupiliwa mbali na Israeli; maana, hayo maji ya farakano hayakunyunyizwa juu yake, atakuwa najisi; unajisi wake ungali upo juu yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Agusaye maiti, yaani mwili wa mtu aliyekufa, asipojitakasa, analitia najisi hema la Mwenyezi-Mungu, naye atatengwa na wana wa Israeli. Mtu huyo atabaki najisi kwa sababu hakunyunyiziwa yale maji ya utakaso.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Agusaye maiti, yaani mwili wa mtu aliyekufa, asipojitakasa, analitia najisi hema la Mwenyezi-Mungu, naye atatengwa na wana wa Israeli. Mtu huyo atabaki najisi kwa sababu hakunyunyiziwa yale maji ya utakaso.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Agusaye maiti, yaani mwili wa mtu aliyekufa, asipojitakasa, analitia najisi hema la Mwenyezi-Mungu, naye atatengwa na wana wa Israeli. Mtu huyo atabaki najisi kwa sababu hakunyunyiziwa yale maji ya utakaso.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Mtu yeyote agusaye maiti ya mtu yeyote na kushindwa kujitakasa mwenyewe hunajisi Maskani ya Mwenyezi Mungu. Mtu huyo ni lazima akatiliwe mbali na Israeli. Kwa sababu hajanyunyiziwa maji ya utakaso, yeye ni najisi; unajisi wake unabaki juu yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Mtu yeyote agusaye maiti ya mtu yeyote na kushindwa kujitakasa mwenyewe hunajisi Maskani ya bwana. Mtu huyo ni lazima akatiliwe mbali na Israeli. Kwa sababu hajanyunyiziwa maji ya utakaso, yeye ni najisi; unajisi wake unabaki juu yake.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

13 Mtu yeyote yule agusaye maiti ya mtu aliyekufa, asijitakase, analitia unajisi maskani ya BWANA; na mtu huyo atatupiliwa mbali na Israeli; maana, hayo maji ya farakano hayakunyunyizwa juu yake, atakuwa najisi; unajisi wake ungali upo juu yake.

Tazama sura Nakili




Hesabu 19:13
27 Marejeleo ya Msalaba  

Mtu yeyote atakayechanganya mafuta mfano wa haya, au mtu yeyote atakayetia mafuta haya juu ya mgeni, mtu huyo atatengwa mbali na watu wake.


Mtu mbaya husukumwa chini katika kutenda mabaya kwake; Bali mwenye haki ana matumaini katika kufa kwake.


Naye akiisha kutakaswa watamhesabia siku saba.


Ni hivi mtakavyowatenga wana wa Israeli na unajisi wao; ili wasife katika unajisi wao, hapo watakapoitia unajisi maskani yangu iliyo katikati yao.


Mimi nami nitamkazia uso wangu mtu huyo, na nitamtenga na watu wake; kwa kuwa ametoa katika kizazi chake na kumpa Moleki, ili kupatia unajisi patakatifu pangu, na kulinajisi jina langu takatifu.


Waambie, Mtu yeyote wa kizazi chenu chote katika vizazi vyenu, atakayevikaribia vile vitu vitakatifu, ambavyo wana wa Israeli wamtakasia BWANA, naye ana unajisi, mtu huyo atatengwa asiwe mbele zangu; mimi ndimi BWANA.


Mtu yeyote wa kizazi cha Haruni aliye na ukoma, au kisonono; asile katika vitu vitakatifu, hata atakapokuwa safi. Tena mtu yeyote atakayekinusa kitu kilicho na unajisi kwa sababu ya wafu, au mtu ambaye shahawa humtoka;


Na kama mtu akifanya dhambi, na kutenda mambo hayo mojawapo ambayo BWANA alizuilia yasifanywe, ajapokuwa hakuyajua, ni mwenye hatia pia, naye atachukua uovu wake.


au kama akiugusa uchafu wa binadamu, uchafu wowote ambao kwao amepata unajisi, bila kujua, hapo apatapo kulijua, ndipo atakapokuwa na hatia;


naye atamletea BWANA sadaka yake ya hatia kwa ajili ya hiyo dhambi yake aliyoifanya, mwana-kondoo wa kike, au mbuzi mke, kutoka katika kundi lake, kuwa ni sadaka ya dhambi; kisha kuhani atamfanyia upatanisho kwa ajili ya hiyo dhambi yake.


lakini mtu huyo atakayekula katika nyama ya sadaka za amani, ambazo ni za BWANA, na unajisi wake akiwa nao juu yake, mtu huyo atakatiliwa mbali na watu wake.


Kisha mtu awaye yote atakapogusa kitu chochote kilicho najisi, uchafu wa binadamu, au mnyama aliye najisi, au machukizo yoyote yaliyo najisi, kisha akala nyama ya dhabihu ya sadaka za amani, ambazo ni za BWANA, mtu huyo atakatiliwa mbali na watu wake.


Lakini mtu afanyaye neno lolote kwa kusudi, kama ni mzalia, kama ni mgeni, huyo amtukana BWANA; na mtu huyo atatupiliwa mbali na watu wake.


Hii ndiyo amri, mtu afapo ndani ya hema; kila mtu aingiaye ndani ya hema hiyo, na kila mtu aliye humo hemani, atakuwa najisi muda wa siku saba.


kisha mtu mmoja aliye safi atatwaa hisopo, na kuitia katika hayo maji naye atayanyunyiza juu ya hema, na juu ya vyombo vyote, na juu ya watu waliokuwapo, na juu yake yeye aliyeugusa mfupa, au mtu aliyeuawa, au mzoga, au kaburi;


na yule aliye safi atamnyunyizia huyo aliye najisi siku ya tatu, na siku ya saba; na katika siku ya saba atamtakasa; naye atazifua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa safi jioni.


Lakini mtu atakayekuwa najisi, naye hataki kujitakasa, mtu huyo atakatiliwa mbali katika mkutano, kwa sababu amepatia unajisi mahali patakatifu pa BWANA; hayo maji ya farakano hayakunyunyizwa juu yake; yeye yuko najisi.


Kisha mtu mmoja aliye safi atayazoa majivu ya huyo ng'ombe, na kuyaweka yawe akiba katika mahali safi nje ya kambi, nayo yatatunzwa kwa ajili ya mkutano wa wana wa Israeli, kuwa ndiyo maji ya farakano; ni sadaka ya dhambi.


Nawe utawafanyia mambo haya ili kuwatakasa; nyunyiza juu yao maji yatakasayo dhambi, nao wajinyoe kwa wembe mwili wote, kisha wazifue nguo zao, na kujitakasa.


Lakini mtu aliye safi, wala hakuwa katika safari, naye amekosa kuishika Pasaka, mtu huyo atatengwa na watu wake; kwa sababu hakumtolea BWANA matoleo kwa wakati wake ulioamriwa, mtu huyo atachukua dhambi yake.


Kwa hiyo niliwaambieni ya kwamba mtakufa katika dhambi zenu; kwa sababu msiposadiki ya kuwa mimi ndiye, mtakufa katika dhambi zenu.


Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho wa neema?


kwa kuwa ni sheria za jinsi ya mwili tu, vyakula na vinywaji na kunawa kwingine kwingine, zilizoamriwa hata wakati wa matengenezo mapya.


Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.


Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa.


Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo