Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Hesabu 18:19 - Swahili Revised Union Version

19 Sadaka zote za kuinuliwa za vitu vitakatifu, wana wa Israeli wavisongezavyo kwa BWANA, nimekupa wewe na wanao na binti zako pamoja nawe, ni haki yenu ya milele; ni agano la chumvi la milele mbele za BWANA kwa ajili yako, na kizazi chako pamoja nawe.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 “Ninakupa wewe, wanao na binti zako, vitu vyote ambavyo watu wa Israeli hunitolea; hivyo ni haki yenu daima. Hili ni agano la milele mbele yangu ambalo ni kwa ajili yako na wazawa wako.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 “Ninakupa wewe, wanao na binti zako, vitu vyote ambavyo watu wa Israeli hunitolea; hivyo ni haki yenu daima. Hili ni agano la milele mbele yangu ambalo ni kwa ajili yako na wazawa wako.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 “Ninakupa wewe, wanao na binti zako, vitu vyote ambavyo watu wa Israeli hunitolea; hivyo ni haki yenu daima. Hili ni agano la milele mbele yangu ambalo ni kwa ajili yako na wazawa wako.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Chochote kitakachotengwa kutoka sadaka takatifu ambazo Waisraeli wanamtolea Mwenyezi Mungu, ninakupa wewe, na wanao wa kiume na wa kike kuwa fungu lenu la milele. Ni agano la milele la chumvi mbele za Mwenyezi Mungu, kwako na wazao wako.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Chochote kitakachotengwa kutoka sadaka takatifu ambazo Waisraeli wanamtolea bwana, ninakupa wewe, wanao na binti zako kama fungu lenu la kawaida. Ni Agano la milele la chumvi mbele za bwana kwako na watoto wako.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

19 Sadaka zote za kuinuliwa za vitu vitakatifu, wana wa Israeli wavisongezavyo kwa BWANA, nimekupa wewe na wanao na binti zako pamoja nawe, ni haki yenu ya milele; ni agano la chumvi la milele mbele za BWANA kwa ajili yako, na kizazi chako pamoja nawe.

Tazama sura Nakili




Hesabu 18:19
15 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini fedha ya matoleo ya kosa, na fedha ya matoleo ya dhambi, haikuletwa nyumbani mwa BWANA; hiyo ilikuwa ya makuhani wenyewe.


je! Haikuwapasa kujua ya kwamba BWANA, Mungu wa Israeli, alimpa Daudi ufalme juu ya Israeli milele, yeye na wanawe kwa agano la chumvi?


Tena akawaamuru watu waliokaa Yerusalemu, watoe sehemu ya makuhani na Walawi, ili hao wajibidiishe katika Torati ya BWANA.


Nawe kitakase kile kidari cha ile sadaka ya kutikiswa, na lile paja la sadaka ya kuinuliwa, lililotikiswa, na lililoinuliwa juu, vya yule kondoo wa kuwekwa kwa kazi takatifu, huyo aliyekuwa kwa ajili ya Haruni, na huyo aliyekuwa kwa ajili ya wanawe;


Nawe utawaleta karibu mbele za BWANA, na makuhani watamwaga chumvi juu yao, nao watawatoa wawe sadaka za kuteketezwa kwa BWANA.


Tena, kila toleo la sadaka yako ya unga utalitia chumvi; wala usiiache sadaka yako ya unga kupungukiwa na chumvi ya agano la Mungu wako; utatoa chumvi pamoja na matoleo yako yote.


Atakula chakula cha Mungu wake, katika hicho kilicho kitakatifu sana, na hicho kilicho kitakatifu.


Na katika hayo atasongeza kimoja katika kila toleo kiwe sadaka ya kuinuliwa kwa BWANA; itakuwa ni ya kuhani atakayeinyunyiza hiyo damu ya sadaka za amani.


Tena kitu hiki ni chako; ile sadaka ya kuinuliwa ya kipawa chao, maana, sadaka za kutikiswa zote za wana wa Israeli; hizi nimekupa wewe, na wanao na binti zako pamoja nawe, ni haki yenu milele; kila mtu katika nyumba yako aliye safi atakula katika hizo.


Kisha BWANA akamwambia Haruni, Tazama, nimekupa wewe ulinzi wa sadaka zangu za kuinuliwa, maana, vitu vyote vya hao wana wa Israeli vilivyowekwa wakfu; nimekupa wewe na wanao vitu hivyo kwa ajili ya kule kutiwa mafuta kwenu, kuwa haki yenu milele.


twaa katika nusu yao, ukampe Eleazari kuhani, kuwa sadaka ya kuinuliwa kwa BWANA.


Basi Musa akampa Eleazari kuhani hiyo sehemu, iliyokuwa sadaka ya kuinuliwa kwa BWANA, kama BWANA alivyomwagiza Musa.


Ila vitu vyako vitakatifu ulivyo navyo, na nadhiri zako, uvitwae uende mahali atakapochagua BWANA;


pelekeni huko sadaka zenu za kuteketezwa, na dhabihu zenu, na zaka zenu, na sadaka ya kuinuliwa ya mikono yenu, na nadhiri zenu, na sadaka zenu za hiari, na wazaliwa wa kwanza wa makundi yenu ya ng'ombe na ya kondoo;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo