Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Hesabu 16:21 - Swahili Revised Union Version

21 Jitengeni ninyi mkaondoke kati ya mkutano huu, ili nipate kuwaangamiza mara moja.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 “Jitengeni na watu hawa, niwaangamize sasa hivi.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 “Jitengeni na watu hawa, niwaangamize sasa hivi.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 “Jitengeni na watu hawa, niwaangamize sasa hivi.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 “Jitengeni na kusanyiko hili ili nipate kuwaangamiza mara moja.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 “Jitengeni kutoka kwenye kusanyiko hili ili nipate kuwaangamiza mara moja.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

21 Jitengeni ninyi mkaondoke kati ya mkutano huu, ili nipate kuwaangamiza mara moja.

Tazama sura Nakili




Hesabu 16:21
19 Marejeleo ya Msalaba  

maana tutapaharibu mahali hapa, kwa kuwa kilio chake kimezidi mbele za BWANA; naye BWANA ametutuma tupaharibu.


Lutu akatoka na kusema na wachumba wa binti zake, akawaambia, “Ondokeni mahali hapa kwa sababu BWANA atauharibu mji huu”. Lakini akaonekana kama achezaye machoni pa wakwe zake.


Namna gani wameangamizwa punde! Wakafutiliwa mbali kwa vitisho.


basi sasa niache, ili hasira zangu ziwake juu yao, niwaangamize, nami nitakufanya wewe uwe taifa kuu.


Kwa nini Wamisri waseme, kuwa “Amewatoa ili awatende mabaya, apate kuwaua milimani na kuwaangamiza watoke juu ya uso wa nchi?” Geuza katika hasira yako kali, ughairi uovu huu ulio nao juu ya watu wako.


BWANA akamwambia Musa, Waambie wana wa Israeli, Ninyi ni watu wenye shingo ngumu; kama mimi nikiingia kati yenu dakika moja, nitawaangamiza; basi sasa vueni mapambo yenu ili nipate kujua nitakalowatenda.


Basi malaika wa BWANA alitoka, akaua watu elfu mia moja na themanini na tano katika kituo cha Waashuri, na watu walipoamka asubuhi na mapema, kumbe, hao walikuwa maiti wote pia.


Podo lao ni kaburi wazi, ni mashujaa wote pia.


Nitawapiga kwa tauni, na kuwaondolea urithi wao, nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, kisha yenye nguvu kuliko wao.


Basi kama wewe ukiwaua watu hawa mfano wa mtu mmoja, ndipo mataifa yaliyosikia habari za sifa zako watakaponena na kusema,


Kisha BWANA akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia,


Ondokeni kati ya mkutano, ili niwaangamize mara moja. Wao wakaanguka kifudifudi.


Kisha BWANA akamwambia Musa, Irudishe fimbo ya Haruni mbele ya ushahidi, ili itunzwe iwe ishara juu ya hawa wana wa maasi; ili uyakomeshe manung'uniko yao waliyoninung'unikia, ili wasife.


Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi.


Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha.


Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo