Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Hesabu 11:23 - Swahili Revised Union Version

23 BWANA akamwambia Musa, Je! Mkono wa BWANA umepungua urefu wake? Sasa utaona kama neno langu litatimizwa kwako, au la.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

23 Mwenyezi-Mungu akamjibu Mose, “Je, uwezo wangu umepungua? Utaona basi kama neno langu litakuwa la kweli kwako au la.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

23 Mwenyezi-Mungu akamjibu Mose, “Je, uwezo wangu umepungua? Utaona basi kama neno langu litakuwa la kweli kwako au la.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

23 Mwenyezi-Mungu akamjibu Mose, “Je, uwezo wangu umepungua? Utaona basi kama neno langu litakuwa la kweli kwako au la.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

23 Mwenyezi Mungu akamjibu Musa, “Je, mkono wa Mwenyezi Mungu ni mfupi sana? Sasa utaona kama jambo nililolisema litatimizwa kwa ajili yako au la.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

23 bwana akamjibu Musa, “Je, mkono wa bwana ni mfupi sana? Sasa utaona kama jambo nililolisema litatimizwa kwa ajili yako au la.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

23 BWANA akamwambia Musa, Je! Mkono wa BWANA umepungua urefu wake? Sasa utaona kama neno langu litatimizwa kwako, au la.

Tazama sura Nakili




Hesabu 11:23
21 Marejeleo ya Msalaba  

Kuna neno gani lililo gumu la kumshinda BWANA? Kwa muhula wake nitakurudia, wakati huu huu mwakani, na Sara atapata mwana wa kiume.


Na mtumishi wake akasema, Je! Niwaandalie hiki watu mia moja? Lakini akasema, Uwape watu, ili wale; kwa kuwa BWANA asema hivi, Watakula na kusaza.


Basi yule afisa, ambaye mfalme alikuwa akitegemea mkono wake, akamjibu yule mtu wa Mungu, akasema, Tazama, kama BWANA angefanya madirisha mbinguni, je! Jambo hili lingewezekana? Akamwambia, Angalia, wewe utaliona kwa macho yako, lakini hutakula.


Wakamjaribu Mungu tena na tena; Na kumkasirisha Mtakatifu wa Israeli.


BWANA akamwambia Musa, Sasa utaona nitakavyomtenda Farao; maana kwa mkono hodari atawapa ruhusa kwenda zao, na kwa mkono hodari atawafukuza katika nchi yake.


Basi, nilipokuja, mbona hapakuwa na mtu? Nilipoita, mbona hapakuwa na mtu aliyenijibu? Je! Mkono wangu ni mfupi, hata nisiweze kukomboa? Au je! Mimi sina nguvu za kuponya? Tazama, kwa kukemea kwangu naikausha bahari, mito ya maji naifanya kuwa jangwa; samaki wao wanuka kwa sababu hapana maji, nao wafa kwa kiu.


Tazama, mkono wa BWANA haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia;


Kwa nini wewe umekuwa kama mtu aliyeshtuka, kama shujaa asiyeweza kuokoa? Lakini wewe, BWANA, u katikati yetu, nasi tunaitwa kwa jina lako; usituache.


Aa! Bwana MUNGU, tazama, wewe umeziumba mbingu na nchi, kwa uweza wako mkuu na kwa mkono wako ulionyoshwa; hapana neno lililo gumu usiloliweza;


Tazama, mimi ni BWANA, Mungu wa wote wenye mwili; je! Kuna neno gumu lolote nisiloliweza?


Maana mimi ni BWANA; mimi nitanena, na neno lile nitakalolinena litatimizwa; wala halitakawilishwa tena; maana katika siku zenu, Ewe nyumba iliyoasi, nitalinena neno hilo na kulitimiza, asema Bwana MUNGU.


Mimi, BWANA, nimenena neno hili, nalo litakuwa; nami nitalifanya; sitaachilia, wala sitahurumia, wala sitajuta; kulingana na njia zako, na kulingana na matendo yako, ndivyo watakavyokuhukumu, asema Bwana MUNGU.


Naye alipolikaribia lile tundu, akamlilia Danieli kwa sauti ya huzuni; mfalme akanena; akamwambia Danieli, Ee Danieli, mtumishi wa Mungu aliye hai, je! Mungu wako, unayemtumikia daima, aweza kukuponya na simba hawa?


Je! Litasemwa neno hili, enyi nyumba ya Yakobo, Roho ya BWANA imepunguzwa? Je! Haya ni matendo yake? Je! Maneno yangu hayamfai yeye aendaye kwa unyofu?


Je! Makundi ya kondoo na ng'ombe yatachinjwa kwa ajili yao, ili kuwatosha? Au samaki wote wa baharini watakusanywa pamoja kwa ajili yao, ili kuwatosha?


Mungu si mtu, aseme uongo; Wala si mwanadamu, ajute; Iwapo amesema, hatalitenda? Iwapo amenena, hatalitimiza?


Yesu akawakazia macho, akawaambia, Kwa wanadamu hilo haliwezekani; bali kwa Mungu yote yawezekana.


Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe.


kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo