Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Hesabu 10:21 - Swahili Revised Union Version

21 Ndipo wakasafiri Wakohathi wenye kuvichukua vile vitu vitakatifu; na hao wengine wakaisimamisha maskani kabla hawajaja wao.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 Kisha walifuata watu wa ukoo wa Kohathi, wakiwa wamebeba vyombo vitakatifu. Walipowasili, hema lilikuwa limekwisha simikwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 Kisha walifuata watu wa ukoo wa Kohathi, wakiwa wamebeba vyombo vitakatifu. Walipowasili, hema lilikuwa limekwisha simikwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 Kisha walifuata watu wa ukoo wa Kohathi, wakiwa wamebeba vyombo vitakatifu. Walipowasili, hema lilikuwa limekwisha simikwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 Kisha Wakohathi wakaondoka, wakichukua vitu vitakatifu. Maskani ilipaswa kusimamishwa kabla wao hawajafika.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 Kisha Wakohathi wakaondoka, wakichukua vitu vitakatifu. Maskani ilikuwa isimamishwe kabla wao hawajafika.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

21 Ndipo wakasafiri Wakohathi wenye kuvichukua vile vitu vitakatifu; na hao wengine wakaisimamisha maskani kabla hawajaja wao.

Tazama sura Nakili

Hesabu 10:21
11 Marejeleo ya Msalaba  

Ndipo Daudi akasema, Haimpasi mtu awaye yote kulichukua sanduku la Mungu, isipokuwa Walawi peke yao; kwa kuwa hao ndio aliowachagua BWANA, ili walichukue sanduku la Mungu, na kumtumikia daima.

Hao walikuwa wana wa Lawi, kwa kufuata koo za baba zao, yaani, vichwa vya koo za baba zao waliohesabiwa, kwa hiyo hesabu ya majina yao, hao walioifanya kazi ya utumishi wa nyumba ya BWANA, wenye miaka ishirini na zaidi.

Tena hapo maskani itakapokwenda mbele, Walawi wataishusha; tena hapo maskani itakaposimamishwa, Walawi wataisimamisha; na mgeni atakayekaribia atauawa.

Na maskani ilishushwa; na wana wa Gershoni, na wana wa Merari, walioichukua maskani, wakasafiri kwenda mbele.

Tena juu ya jeshi la kabila la wana wa Gadi ni Eliasafu mwana wa Deueli.

Ndipo hema ya kukutania itasafiri, pamoja na kambi za Walawi katikati ya kambi zote; kama wapangavyo kambi, watasafiri vivyo hivyo, kila mtu mahali pake, penye bendera zao.

lakini wasiingie wao kupaona mahali pale patakatifu, hata kwa dakika moja, ili wasife.

Lakini hakuwapa wana wa Kohathi; maana, utumishi wa vile vitu vitakatifu ulikuwa ni wao; nao wakavichukua mabegani mwao.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo