Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Ezra 9:3 - Swahili Revised Union Version

3 Nami niliposikia hayo, nikararua nguo yangu na joho langu, nikang'oa nywele za kichwa changu, na ndevu zangu, nikaketi kwa mshangao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Nilipoyasikia maelezo hayo, nilizirarua nguo zangu na joho langu, nikazingoa nywele zangu na ndevu zangu kwa huzuni kubwa na kuketi chini kwa hofu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Nilipoyasikia maelezo hayo, nilizirarua nguo zangu na joho langu, nikazingoa nywele zangu na ndevu zangu kwa huzuni kubwa na kuketi chini kwa hofu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Nilipoyasikia maelezo hayo, nilizirarua nguo zangu na joho langu, nikazing'oa nywele zangu na ndevu zangu kwa huzuni kubwa na kuketi chini kwa hofu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Niliposikia jambo hili nilirarua koti langu na joho langu, nikazing’oa nywele za kichwa changu na ndevu zangu na kuketi nikishangaa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Niliposikia jambo hili nilirarua koti langu na joho langu, nikazing’oa nywele za kichwa changu na ndevu zangu na kuketi nikishangaa.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

3 Nami niliposikia hayo, nikararua nguo yangu na joho langu, nikang'oa nywele za kichwa changu, na ndevu zangu, nikaketi kwa mshangao.

Tazama sura Nakili




Ezra 9:3
21 Marejeleo ya Msalaba  

Ndipo Daudi akashika nguo zake akazirarua na kadhalika watu wote waliokuwa pamoja naye;


Ndipo Eliakimu, mwana wa Hilkia, aliyekuwa msimamizi wa nyumba ya mfalme, na Shebna, mwandishi, na Yoa, mwana wa Asafu, mwenye kuandika tarehe, wakaenda kwa Hezekia, na nguo zao zimeraruliwa, wakamwambia maneno ya yule kamanda.


Hapo niliposikia maneno hayo, nikaketi, nikalia, nikaomboleza siku kadhaa; kisha nikafunga, nikaomba mbele za Mungu wa mbinguni;


Nikagombana nao, nikawalaani, nikawapiga baadhi yao, na kuwang'oa nywele zao; nikawaapisha kwa Mungu, nikasema, Msiwaoze wana wao binti zenu, wala msiwatwae binti zao ili waolewe na wana wenu, wala na ninyi wenyewe.


Ndipo Ayubu akainuka, akalirarua joho lake, kisha akanyoa kichwa chake, na kuanguka chini, na kusujudia;


Ghadhabu kuu imenishika kwa sababu ya wasio haki, Waiachao sheria yako.


Na roho yangu imezimia ndani yangu, Moyo wangu ndani yangu umeshtuka.


Mwambieni Mungu, Matendo yako yatisha kama nini! Kwa ajili ya wingi wa nguvu zako, Adui zako watakuja kunyenyekea mbele zako.


Wanapanda juu hata Bayithi na Diboni, mpaka mahali palipo juu ili walie; juu ya Nebo na juu ya Medeba Wamoabi wanalia; Wana upaa juu ya vichwa vyao vyote; kila ndevu zimenyolewa.


Lakini hawakuogopa, wala hawakurarua mavazi yao, wala mfalme, wala watumishi wake hata mmoja waliosikia maneno hayo yote.


Zikate nywele zako, Ee Yerusalemu, uzitupe, Ukafanye maombolezo juu ya vilele vya milima; Kwa maana BWANA amekikataa na kukitupa Kizazi cha ghadhabu yake.


Ndipo nikawafikia watu waliohamishwa, huko Tel-abibu, waliokuwa wakikaa karibu na mto Kebari, nikafika huko walikokuwa wakikaa; nikaketi huko miongoni mwao muda wa siku saba, katika hali ya ushangao mwingi.


Tena watajifungia nguo za magunia, na utisho utawafunika; na aibu itakuwa juu ya nyuso zote, na upaa juu ya vichwa vyao vyote.


Ndipo Danieli, aliyeitwa jina lake Belteshaza, akashangaa kwa muda, na fikira zake zikamfadhaisha. Mfalme akajibu akasema, Ee Belteshaza, ndoto ile isikufadhaishe wala tafsiri yake. Belteshaza akajibu, akasema, Bwana wangu, ndoto hii iwapate wao wakuchukiao, na tafsiri yake iwapate adui zako.


Na mimi, Danieli, nikazimia, nikaugua siku kadhaa; kisha nikaondoka, nikatenda shughuli za mfalme; nami niliyastajabia yale maono, ila hakuna aliyeyafahamu.


Wasijifanyie upara kichwani, wala wasinyoe pembe za ndevu zao, wala wasichanje tojo katika miili yao.


Jinyoeni upara, jikateni nywele zenu, Kwa ajili ya watoto waliowafurahisha; Panueni upara wenu kama tai; Kwa maana wamekwenda mbali nanyi uhamishoni.


Yoshua akararua mavazi yake, akaanguka kifudifudi mbele ya sanduku la BWANA hadi jioni, yeye na wazee wa Israeli; wakatia mavumbi vichwani mwao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo