Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Ezra 8:20 - Swahili Revised Union Version

20 na katika Wanethini, ambao Daudi, na wakuu, walikuwa wamewaweka kwa ajili ya utumishi wa Walawi, Wanethini mia mbili na ishirini; wote wametajwa kwa majina yao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

20 Mbali na hao, kulikuwa na wahudumu wa hekalu 220 ambao babu zao walikuwa wamechaguliwa na mfalme Daudi na maofisa wake kuwasaidia Walawi. Majina ya watu wote hawa yaliorodheshwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

20 Mbali na hao, kulikuwa na wahudumu wa hekalu 220 ambao babu zao walikuwa wamechaguliwa na mfalme Daudi na maofisa wake kuwasaidia Walawi. Majina ya watu wote hawa yaliorodheshwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

20 Mbali na hao, kulikuwa na wahudumu wa hekalu 220 ambao babu zao walikuwa wamechaguliwa na mfalme Daudi na maofisa wake kuwasaidia Walawi. Majina ya watu wote hawa yaliorodheshwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

20 Vilevile walileta watumishi wa Hekalu mia mbili na ishirini, kikundi ambacho Daudi na maafisa walikuwa wamekianzisha ili kusaidia Walawi. Wote waliorodheshwa kwa majina.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

20 Vilevile walileta watumishi wa Hekalu 220, kikundi ambacho Daudi na maafisa walikuwa wamekiweka kusaidia Walawi. Wote walikuwa wameorodheshwa kwa majina.

Tazama sura Nakili




Ezra 8:20
7 Marejeleo ya Msalaba  

Basi wenyeji wa kwanza waliokaa katika miliki yao katika miji yao walikuwa Israeli, na makuhani, na Walawi, na Wanethini.


Wanethini; wazawa wa Siha, wazawa wa Hasufa, wazawa wa Tabaothi;


Nao wakakwea baadhi ya wana wa Israeli, na wa makuhani, na wa Walawi, na waimbaji, na mabawabu, na Wanethini, ili kwenda Yerusalemu, katika mwaka wa saba wa mfalme Artashasta.


Nikawatuma kwa Ido, mkuu, huko Kasifia; nikawaambia watakayomwambia Ido, na ndugu zake hao Wanethini, huko Kasifia, kwamba watuletee watu watakaohudumu katika nyumba ya Mungu wetu.


na Hashabia, na pamoja naye Yeshaya, wa wana wa Merari, na ndugu zake na wana wao, watu ishirini;


Nawe utawapa Haruni na wanawe hao Walawi wawe nao; amepewa watu hao kabisa kwa ajili ya wana wa Israeli.


Naam, nataka na wewe pia, mtumwa mwenzangu wa kweli, uwasaidie wanawake hao; kwa maana waliishindania Injili pamoja nami, na Klementi naye, na wale wengine waliofanya kazi pamoja nami, ambao majina yao yamo katika kitabu cha uzima.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo