Ezra 3:11 - Swahili Revised Union Version11 Wakaimbiana, wakimhimidi BWANA, na kumshukuru, wakasema, Kwa kuwa ni mwema, kwa maana fadhili zake kwa Israeli ni za milele. Kisha watu wote wakapaza sauti zao, na kupiga kelele, walipomhimidi BWANA, kwa sababu msingi wa nyumba ya BWANA umekwisha kuwekwa. Tazama suraMatoleo zaidiBiblia Habari Njema11 Waliimba kwa kupokezana, wakimsifu na kumtukuza Mwenyezi-Mungu: “Kwa kuwa yu mwema, fadhili zake kwa Israeli zadumu milele.” Watu wote walipaza sauti kwa nguvu zao zote, wakamsifu Mwenyezi-Mungu kwa sababu ya kuanza kujengwa msingi wa nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Tazama suraBiblia Habari Njema - BHND11 Waliimba kwa kupokezana, wakimsifu na kumtukuza Mwenyezi-Mungu: “Kwa kuwa yu mwema, fadhili zake kwa Israeli zadumu milele.” Watu wote walipaza sauti kwa nguvu zao zote, wakamsifu Mwenyezi-Mungu kwa sababu ya kuanza kujengwa msingi wa nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Tazama suraBiblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza11 Waliimba kwa kupokezana, wakimsifu na kumtukuza Mwenyezi-Mungu: “Kwa kuwa yu mwema, fadhili zake kwa Israeli zadumu milele.” Watu wote walipaza sauti kwa nguvu zao zote, wakamsifu Mwenyezi-Mungu kwa sababu ya kuanza kujengwa msingi wa nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Tazama suraNeno: Bibilia Takatifu11 Waliimba nyimbo za sifa na za shukrani kwa Mwenyezi Mungu hivi: “Yeye ni mwema; upendo wake kwa Israeli wadumu milele.” Watu wote wakapaza sauti kubwa za sifa kwa Mwenyezi Mungu, kwa sababu msingi wa nyumba ya Mwenyezi Mungu ulikuwa umewekwa. Tazama suraNeno: Maandiko Matakatifu11 Waliimba nyimbo za sifa na za shukrani kwa bwana hivi: “Yeye ni mwema; upendo wake kwa Israeli wadumu milele.” Watu wote wakapaza sauti kubwa za sifa kwa bwana, kwa sababu msingi wa nyumba ya bwana ulikuwa umewekwa. Tazama suraBIBLIA KISWAHILI11 Wakaimbiana, wakimhimidi BWANA, na kumshukuru, wakasema, Kwa kuwa ni mwema, kwa maana fadhili zake kwa Israeli ni za milele. Kisha watu wote wakapaza sauti zao, na kupiga kelele, walipomhimidi BWANA, kwa sababu msingi wa nyumba ya BWANA umekwisha kuwekwa. Tazama sura |
hata ikawa, wenye panda na waimbaji walipokuwa kama mmoja, wakisikizisha sauti moja ya kumsifu na kumshukuru BWANA nao wakipaza sauti pamoja na panda na matoazi na vinanda, wakimsifu BWANA, wakisema, Kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake ni za milele; ndipo nyumba ikajawa na wingu, naam, nyumba ya BWANA,
itasikika tena sauti ya furaha na sauti ya shangwe, sauti ya bwana arusi na sauti ya bibi arusi, sauti yao wasemao Mshukuruni BWANA wa majeshi, maana BWANA ni mwema, rehema zake ni za milele; na sauti zao waletao sadaka za shukrani nyumbani kwa BWANA. Kwa kuwa nitawarudisha wafungwa wa nchi hii kama kwanza, asema BWANA.