Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Ezra 1:5 - Swahili Revised Union Version

5 Ndipo wakaondoka wakuu wa koo za mababa, wa Yuda na Benyamini, na makuhani, na Walawi, naam, watu wote ambao Mungu ameamsha roho zao kukwea, ili kuijenga nyumba ya BWANA, iliyoko Yerusalemu.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Basi, wakaondoka viongozi wa koo za makabila ya Yuda na Benyamini, makuhani na Walawi, na kila mtu ambaye Mungu alimpa moyo wa kwenda kujenga upya nyumba ya Mwenyezi-Mungu, iliyoko Yerusalemu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Basi, wakaondoka viongozi wa koo za makabila ya Yuda na Benyamini, makuhani na Walawi, na kila mtu ambaye Mungu alimpa moyo wa kwenda kujenga upya nyumba ya Mwenyezi-Mungu, iliyoko Yerusalemu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Basi, wakaondoka viongozi wa koo za makabila ya Yuda na Benyamini, makuhani na Walawi, na kila mtu ambaye Mungu alimpa moyo wa kwenda kujenga upya nyumba ya Mwenyezi-Mungu, iliyoko Yerusalemu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Kisha viongozi wa jamaa ya Yuda na Benyamini na makuhani na Walawi kila mmoja ambaye moyo wake ulisukumwa na Mungu, akajiandaa kupanda ili kuijenga nyumba ya Mwenyezi Mungu huko Yerusalemu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Kisha viongozi wa jamaa ya Yuda na Benyamini na makuhani na Walawi kila mmoja ambaye moyo wake ulisukumwa na Mungu, akajiandaa kupanda ili kuijenga nyumba ya bwana huko Yerusalemu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

5 Ndipo wakaondoka wakuu wa koo za mababa, wa Yuda na Benyamini, na makuhani, na Walawi, naam, watu wote ambao Mungu ameamsha roho zao kukwea, ili kuijenga nyumba ya BWANA, iliyoko Yerusalemu.

Tazama sura Nakili

Ezra 1:5
11 Marejeleo ya Msalaba  

Ikawa katika mwaka wa kwanza wa Koreshi, mfalme wa Uajemi, ili kwamba neno la BWANA alilolisema kwa kinywa cha Yeremia lipate kutimizwa, BWANA akamwamsha roho yake Koreshi, mfalme wa Uajemi, hata akapiga mbiu katika ufalme wake wote, akaiandika pia, akisema,

Ikawa katika mwaka wa kwanza wa Koreshi, mfalme wa Uajemi, ili kwamba neno la BWANA alilolisema kwa kinywa cha Yeremia lipate kutimizwa, BWANA akaamsha roho yake Koreshi, mfalme wa Uajemi, hata akapiga mbiu katika ufalme wake wote, akaiandika pia, akisema,

Koreshi, mfalme wa Uajemi asema hivi; BWANA, Mungu wa mbinguni, amenipa falme zote za dunia; naye ameniagiza nimjengee nyumba katika Yerusalemu, ulioko Yuda.

Na mtu yeyote aliyesalia mahali popote akaapo kama mgeni, na asaidiwe na watu wa mahali pake, kwa fedha, na dhahabu, na mali, na wanyama, zaidi ya vitu vitolewavyo kwa hiari ya mtu, kwa ajili ya nyumba ya Mungu, iliyoko Yerusalemu.

Kisha nikaondoka usiku, mimi pamoja na watu wachache; wala sikumwambia mtu neno hili alilolitia Mungu wangu moyoni mwangu, nilitende kwa ajili ya Yerusalemu; wala hapakuwa na mnyama pamoja nami, ila mnyama yule niliyempanda mwenyewe.

Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu; Bali jawabu la ulimi hutoka kwa BWANA.

BWANA akaiamsha roho ya Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, mtawala wa Yuda, na roho ya Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, na roho za watu waliokuwa wamebaki; wakaenda, wakafanya kazi katika nyumba ya BWANA wa majeshi, Mungu wao;

Lakini ahimidiwe Mungu atiaye bidii ile ile kwa ajili yenu katika moyo wa Tito.

Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema.

Mpenzi, usiuige ubaya, bali uige wema. Yeye atendaye mema ni wa Mungu, bali yeye atendaye mabaya hakumwona Mungu.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo