Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Ezekieli 7:3 - Swahili Revised Union Version

3 Sasa mwisho huu unakupata, nami nitakuletea hasira yangu, nitakuhukumu kulingana na njia zako; nami nitakupatiliza machukizo yako yote.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Sasa mwisho umewafikia; sasa mtausikia ukali wa hasira yangu juu yenu. Nitawahukumu kadiri ya mwenendo wenu. Nitawaadhibu kwa machukizo yenu yote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Sasa mwisho umewafikia; sasa mtausikia ukali wa hasira yangu juu yenu. Nitawahukumu kadiri ya mwenendo wenu. Nitawaadhibu kwa machukizo yenu yote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Sasa mwisho umewafikia; sasa mtausikia ukali wa hasira yangu juu yenu. Nitawahukumu kadiri ya mwenendo wenu. Nitawaadhibu kwa machukizo yenu yote.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Sasa mwisho umekuja juu yenu, nami nitamwaga hasira yangu dhidi yenu. Nitawahukumu sawasawa na matendo yenu na kuwalipiza kwa ajili ya desturi zenu zote za kuchukiza.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Sasa mwisho umekuja juu yenu nami nitamwaga hasira yangu dhidi yenu. Nitawahukumu sawasawa na matendo yenu na kuwalipiza kwa ajili ya desturi zenu zote za kuchukiza.

Tazama sura Nakili




Ezekieli 7:3
27 Marejeleo ya Msalaba  

Mungu akamwambia Nuhu, Mwisho wa kila kiumbe umefika mbele zangu; kwa sababu wameijaza dunia maovu, basi nitawaangamiza pamoja na dunia.


Ukasema, Mimi nitakuwa malkia milele; hata hukuyatia hayo moyoni mwako, wala hukukumbuka mwisho wa mambo hayo.


Nitawagonganisha, mtu na mwenzake, naam, baba za watu na watoto wao pamoja, asema BWANA; sitahurumia, wala sitaachilia, wala sitarehemu, hata nisiwaangamize.


Bali wao ambao mioyo yao huenda kwa kuufuata moyo wa vitu vyao vichukizavyo, na machukizo yao, nitaileta njia yao iwajilie juu ya vichwa vyao, asema Bwana MUNGU.


Nami nitakuhukumu, kama wahukumiwavyo wake walioolewa wazinio, na kumwaga damu, nami nitakupatiliza damu ya ghadhabu na wivu.


Kwa sababu hukuzikumbuka siku za ujana wako, bali umenikasirisha kwa mambo hayo yote; basi, tazama, mimi nami nitaleta matendo yako juu ya kichwa chako, asema Bwana MUNGU; wala hutafanya uasherati zaidi ya machukizo yako yote.


Maana Bwana MUNGU asema hivi; Nitakutenda vile vile kama ulivyotenda, uliyekidharau kiapo kwa kulivunja agano.


Basi, nitawahukumu ninyi, nyumba ya Israeli, kila mmoja kwa kadiri ya njia zake, asema Bwana MUNGU. Rudini, mkaghairi, na kuyaacha makosa yenu yote; basi hivyo uovu wenu hautakuwa uharibifu wenu.


Na wewe, Ewe mtu mwovu, uliyetiwa jeraha kiasi cha kukuua, mkuu wa Israeli, ambaye siku yako imekuja, katika wakati wa uovu wa mwisho;


Kwa sababu hiyo nimemwaga ghadhabu yangu juu yao; nimewateketeza kwa moto wa hasira yangu; nami nimeileta njia yao wenyewe juu ya vichwa vyao, asema Bwana MUNGU.


Mimi, BWANA, nimenena neno hili, nalo litakuwa; nami nitalifanya; sitaachilia, wala sitahurumia, wala sitajuta; kulingana na njia zako, na kulingana na matendo yako, ndivyo watakavyokuhukumu, asema Bwana MUNGU.


Lakini ninyi husema, Njia ya Bwana si sawa. Ee nyumba ya Israeli, nitawahukumu ninyi; kila mtu kwa kadiri ya njia zake.


Nikawatawanya katika mataifa, wakatapanyika katika nchi nyingi; kwa kadiri ya njia yao, na kwa kadiri ya matendo yao, niliwahukumu.


Theluthi yenu mtakufa kwa tauni, na kwa njaa watakomeshwa ndani yako; na theluthi yenu wataanguka kwa upanga pande zako zote; na theluthi yenu nitawatawanya kwa pepo zote, kisha nitafuta upanga nyuma yao.


Hivyo ndivyo ghadhabu yangu itakavyotimia, nami nitatosheleza hasira yangu juu yao, nami nitafarijika; nao watajua ya kuwa mimi, BWANA, nimenena kwa wivu wangu, nitakapokuwa nimeitimiza ghadhabu yangu juu yao.


Na wewe, mwanadamu, Bwana MUNGU aiambia hivi nchi ya Israeli; Ni mwisho; mwisho umezijia pembe nne za nchi.


Mfalme ataomboleza, na mkuu atavikwa ukiwa, na mikono ya watu wa nchi itataabika; nitawatenda kulingana na njia yao; nami nitawahukumu kulingana na kustahili kwao; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.


Jicho langu halitakuachilia, wala sitaona huruma; bali nitakupatiliza njia zako, na machukizo yako yatakuwa katikati yako; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.


Nami, jicho langu halitaachilia, wala sitakuwa na huruma; lakini nitaleta njia yao juu ya vichwa vyao.


Tumboni alimshika ndugu yake kisigino; Na alipokuwa mtu mzima alishindana na Mungu;


Akaniambia, Amosi, unaona nini? Nikasema, Naona kikapu cha matunda ya wakati wa joto. Ndipo BWANA akaniambia, Mwisho wao watu wangu Israeli umewajia; sitawapita tena kamwe.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo