Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Ezekieli 4:3 - Swahili Revised Union Version

3 Kisha ukajipatie bamba la chuma, ukalisimamishe liwe ukuta wa chuma kati ya wewe na mji huo; ukaelekeze uso wako juu yake, nao utahusuriwa, nawe utauhusuru. Hili litakuwa ishara kwa nyumba ya Israeli.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Kisha, chukua bamba la chuma ulisimamishe liwe kama ukuta wa chuma kati yako na mji. Kisha uelekee mji huo unaozingirwa, uoneshe kana kwamba unazingirwa. Fanya alama ya kuuzingira. Hii itakuwa ishara kwa taifa la Israeli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Kisha, chukua bamba la chuma ulisimamishe liwe kama ukuta wa chuma kati yako na mji. Kisha uelekee mji huo unaozingirwa, uoneshe kana kwamba unazingirwa. Fanya alama ya kuuzingira. Hii itakuwa ishara kwa taifa la Israeli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Kisha, chukua bamba la chuma ulisimamishe liwe kama ukuta wa chuma kati yako na mji. Kisha uelekee mji huo unaozingirwa, uoneshe kana kwamba unazingirwa. Fanya alama ya kuuzingira. Hii itakuwa ishara kwa taifa la Israeli.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Kisha chukua bamba la chuma, ukalisimamishe liwe kama ukuta wa chuma kati yako na huo mji, nawe uuelekeze uso wako. Huo mji utakuwa katika hali ya kuzingirwa, nawe ndiwe utakayeuzingira. Hii itakuwa ishara kwa nyumba ya Israeli.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Kisha chukua bamba la chuma, ukalisimamishe liwe kama ukuta wa chuma kati yako na huo mji, nawe uuelekeze uso wako. Huo mji utakuwa katika hali ya kuzingirwa, nawe utauzingira. Hii itakuwa ishara kwa nyumba ya Israeli.

Tazama sura Nakili




Ezekieli 4:3
13 Marejeleo ya Msalaba  

Naye akafanya hivyo akaenda uchi, miguu yake ikiwa haina viatu. BWANA akasema, Kama vile mtumishi wangu Isaya anavyokwenda uchi, bila viatu, awe ishara na ajabu kwa muda wa miaka mitatu juu ya Misri na juu ya Kushi;


Hata ikawa mabonde yako mateule yamejaa magari ya vita, nao wapandao farasi wamejipanga katika malango.


Angalieni, mimi na watoto hawa niliopewa na BWANA tu ishara na ajabu katika Israeli, zitokazo kwa BWANA wa majeshi, yeye akaaye katika mlima Sayuni.


Hata ikawa, Yerusalemu ulipotwaliwa, (katika mwaka wa tisa wa Sedekia, mfalme wa Yuda, katika mwezi wa kumi, Nebukadneza, mfalme wa Babeli, na jeshi lake lote, wakaja juu ya Yerusalemu, wakauzingira;


katika mwaka wa kumi na mmoja wa Sedekia, mwezi wa nne, siku ya tisa ya mwezi, sehemu ya ukuta wa mji ilibomolewa;)


Sema, Mimi ni ishara kwenu; kama mimi nilivyotenda, wao nao watatendwa vile vile; watahamishwa, watakwenda kufungwa.


Mbele ya macho yao utajitwika begani pako, na kuvichukua nje gizani; utafunika uso wako, hata usiione nchi; kwa maana nimekuweka uwe ishara kwa nyumba ya Israeli.


Theluthi ya hizo utaiteketeza katikati ya mji, siku za kuzingirwa zitakapomalizika; nawe utatwaa theluthi, na kuipiga kwa upanga pande zote; nawe utatawanya theluthi ichukuliwe na upepo, nami nitafuta upanga nyuma yake.


Naye atakaza uso wake ili aje pamoja na nguvu zote za ufalme wake, naye atafanya mapatano naye; naye atatenda kadiri apendavyo; naye atampa binti amuoe, ili hatimaye amwangamize huyo mfalme; lakini hataweza kumwangamiza.


Tena matoleo yako kwamba ni sadaka ya unga wa kaangoni, yatakuwa ya unga mwembamba usiotiwa chachu, uliokandwa kwa mafuta.


Simeoni akawabariki, akamwambia Mariamu mama yake, Tazama, huyu amewekwa kwa kuanguka na kuinuka wengi walio katika Israeli, na kuwa ishara itakayonenewa.


Mungu naye akishuhudia pamoja nao kwa ishara na ajabu na nguvu za namna nyingi, na kwa karama za Roho Mtakatifu, kama alivyopenda mwenyewe.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo