Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Esta 7:3 - Swahili Revised Union Version

3 Ndipo malkia Esta alipojibu, akasema, Ikiwa nimepata kibali machoni pako, Ewe Mfalme, na ikimpendeza mfalme, hebu nipewe maisha yangu kwa ombi langu, na watu wangu kwa maombi yangu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Malkia Esta akamjibu, “Kama nimepata upendeleo kwako, ewe mfalme, na ukiwa radhi kunitimizia ombi langu, haja yangu ni mimi niishi na watu wangu pia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Malkia Esta akamjibu, “Kama nimepata upendeleo kwako, ewe mfalme, na ukiwa radhi kunitimizia ombi langu, haja yangu ni mimi niishi na watu wangu pia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Malkia Esta akamjibu, “Kama nimepata upendeleo kwako, ewe mfalme, na ukiwa radhi kunitimizia ombi langu, haja yangu ni mimi niishi na watu wangu pia.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Kisha Malkia Esta akajibu, “Kama nimepata kibali kwako, ee mfalme, tena kama inapendeza utukufu wako, nijalie maisha yangu, hii ndiyo haja yangu. Pia uokoe watu wangu, hili ndilo ombi langu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Kisha Malkia Esta akajibu, “Kama nimepata kibali kwako, ee mfalme, tena kama inapendeza utukufu wako, nijalie maisha yangu, hii ndiyo haja yangu. Pia uokoe watu wangu, hili ndilo ombi langu.

Tazama sura Nakili

Swahili Roehl Bible 1937

3 Ndipo, Esteri, mkewe mfalme, alipomjibu akisema: Kama nimeona upendeleo mbele yako, mfalme, navyo vikiwa vema kwako, mfalme, nipewe roho yangu kwa kuomba kwangu! Tena nipewe wenzangu wa ukoo kwa kutaka kwangu!

Tazama sura Nakili




Esta 7:3
9 Marejeleo ya Msalaba  

Watumwa wake wakamwambia, Angalia sasa, tumesikia ya kuwa wafalme wa nyumba ya Israeli ni wafalme wenye rehema; tafadhali, tuvae magunia viunoni, na kamba vichwani, tumtokee mfalme wa Israeli; labda atakuokoa roho yako.


Tena akatuma kamanda wa hamsini wa tatu, pamoja na hamsini wake. Yule kamanda wa hamsini wa tatu akapanda, akaenda akapiga magoti mbele ya Eliya, akamsihi sana, akamwambia, Ee mtu wa Mungu, nakusihi, roho yangu, na roho za watumishi wako hawa hamsini, ziwe na thamani machoni pako.


Pia akampa na nakala ya andiko la mbiu ya kuwaangamiza, iliyotangazwa Shushani, ili amwoneshe Esta, na kumweleza; tena amwagize aingie kwa mfalme, kumsihi na kuwaombea watu wake.


Ikiwa nimepata kibali machoni pa mfalme, na mfalme akiona vema kunipa niombalo, na kunitimizia haja yangu, na aje tena mfalme na Hamani kwenye karamu nitakayowaandalia, nami kesho nitafanya kama vile mfalme alivyosema.


Mfalme akaondoka kwa ghadhabu kutoka kwenye karamu ya divai, akaingia bustani ya ngome. Hamani naye akasimama ili ajitakie maisha yake kwa malkia Esta; kwa kuwa aliona ya kwamba amekusudiwa madhara na mfalme.


Akasema, Mfalme akiona vema, nami nikiwa nimepata kibali machoni pake, na neno likionekana jema mbele ya mfalme, nami nikimpendeza machoni pake, na iandikwe amri kuzitangua barua za Hamani mwana wa Hamedatha, Mwagagi, alizotunga na kuziandika ili kuwaangamiza Wayahudi walioko katika mikoa yote ya mfalme.


Shetani akamjibu BWANA, na kusema, Ngozi kwa ngozi, naam, yote aliyo nayo mtu atayatoa kwa ajili ya uhai wake.


basi, utawaambia, Nilimwomba mfalme asinirudishe nyumbani kwa Yonathani, nisije nikafa humo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo