Esta 3:11 - Swahili Revised Union Version11 Kisha mfalme akamwambia Hamani, Hiyo fedha umepewa, na watu pia, fanya uonavyo vema. Tazama suraMatoleo zaidiBiblia Habari Njema11 Ndipo mfalme akamwambia Hamani, “Umepewa watu wote na hizo fedha, tumia upendavyo.” Tazama suraBiblia Habari Njema - BHND11 Ndipo mfalme akamwambia Hamani, “Umepewa watu wote na hizo fedha, tumia upendavyo.” Tazama suraBiblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza11 Ndipo mfalme akamwambia Hamani, “Umepewa watu wote na hizo fedha, tumia upendavyo.” Tazama suraNeno: Bibilia Takatifu11 Mfalme akamwambia Hamani, “Baki na fedha yako na uwatendee hao watu utakavyo.” Tazama suraNeno: Maandiko Matakatifu11 Mfalme akamwambia Hamani, “Baki na fedha yako na uwatendee hao watu utakavyo.” Tazama sura |
Basi, waandishi wa mfalme wakaitwa, siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kwanza; na barua zikaandikwa, kama vile Hamani alivyoagiza, kwa wakuu wa mfalme, na wakuu wa mikoa, na wakuu wa kila taifa; kila mkoa kwa mwandiko wake, na kila taifa kwa lugha yake; zikaandikwa kwa jina la mfalme Ahasuero, na kutiwa mhuri kwa pete yake.
Na sasa, tazama, nakufungulia leo minyororo hii iliyo mikononi mwako. Kama ukiona ni vema kwenda Babeli pamoja nami, haya! Njoo, nami nitakutunza sana; lakini kama ukiona ni vibaya kwenda Babeli pamoja nami, basi, acha; tazama, nchi yote iko mbele yako; palipo pema machoni pako na pa kukufaa, nenda huko.