Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Danieli 9:20 - Swahili Revised Union Version

20 Basi hapo nilipokuwa nikisema, na kuomba, na kuiungama dhambi yangu, na dhambi ya watu wangu Israeli, na kuomba dua yangu mbele za BWANA, Mungu wangu, kwa ajili ya mlima mtakatifu wa Mungu wangu;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

20 “Basi, nilipokuwa nikiomba, nikiungama dhambi zangu na dhambi za watu wangu wa Israeli, pamoja na kumsihi Mwenyezi-Mungu kwa ajili ya mlima wake mtakatifu,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

20 “Basi, nilipokuwa nikiomba, nikiungama dhambi zangu na dhambi za watu wangu wa Israeli, pamoja na kumsihi Mwenyezi-Mungu kwa ajili ya mlima wake mtakatifu,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

20 “Basi, nilipokuwa nikiomba, nikiungama dhambi zangu na dhambi za watu wangu wa Israeli, pamoja na kumsihi Mwenyezi-Mungu kwa ajili ya mlima wake mtakatifu,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

20 Basi, nilipokuwa bado nikinena na kuomba, nikiungama dhambi yangu na dhambi ya watu wangu Israeli, na nikifanya maombi yangu kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wangu, kwa ajili ya mlima wake mtakatifu,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

20 Basi, nilipokuwa bado nikinena na kuomba, nikiungama dhambi yangu na dhambi ya watu wangu Israeli, na nikifanya maombi yangu kwa bwana Mwenyezi Mungu wangu kwa ajili ya mlima wake mtakatifu,

Tazama sura Nakili

Swahili Roehl Bible 1937

20 Nilipokuwa ninasema bado nikiomba na kuyaungama makosa yangu na makosa yao walio ukoo wangu wa Isiraeli na kuyatoa malalamiko yangu usoni pa Bwana Mungu wangu kwa ajili ya mlima mtakatifu wa Mungu wangu,

Tazama sura Nakili




Danieli 9:20
24 Marejeleo ya Msalaba  

Basi hapo Ezra alipokuwa akiomba na kuungama, akilia, na kujiangusha kifudifudi mbele ya nyumba ya Mungu, kusanyiko kubwa sana la wanaume, wanawake na watoto, kutoka katika Israeli likamkusanyikia; maana watu hao walikuwa wakilia sana.


tega sikio lako, macho yako yakafumbuke, upate kuyasikiliza maombi ya mtumishi wako, ninayoomba mbele zako wakati huu, mchana na usiku, kwa ajili ya wana wa Israeli, watumishi wako; hapo ninapoziungama dhambi za wana wa Israeli, tulizozifanya juu yako; naam, mimi na nyumba ya baba yangu tumefanya dhambi.


BWANA yuko karibu na wote wamwitao, Wote wamwitao kwa uaminifu.


Ndipo nikakuungamia dhambi yangu, Wala sikuuficha upotovu wangu. Nilisema, Nitayakiri maasi yangu kwa BWANA, Nawe ukanisamehe upotovu wa dhambi yangu.


Bila shaka hakuna mwanadamu mwenye haki hapa duniani, atendaye mema pasipo kutenda dhambi.


Nitawaleta hao nao hadi katika mlima wangu mtakatifu, na kuwafurahisha katika nyumba yangu ya sala; makafara yao na dhabihu zao zitakubaliwa juu ya madhabahu zangu; kwa maana nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote.


Ndipo utaita, na BWANA ataitika; utalia, naye atasema, Mimi hapa. Kama ukiiondoa nira; isiwepo kati yako, wala kunyosha kidole, wala kunena maovu;


Ndipo niliposema, Ole wangu! Kwa maana nimepotea; kwa sababu mimi ni mtu mwenye midomo michafu, nami ninakaa kati ya watu wenye midomo michafu; na macho yangu yamemwona Mfalme, BWANA wa majeshi.


Na itakuwa ya kwamba, kabla hawajaomba, nitajibu; na wakiwa bado wanena, nitasikia.


Ndipo akaniambia, Usiogope, Danieli; kwa maana tangu siku ile ya kwanza ulipotia moyo wako ufahamu, na kujinyenyekeza mbele za Mungu wako, maneno yako yalisikiwa; nami nimekuja kwa ajili ya maneno yako.


Katika siku zile mimi, Danieli, nilikuwa nikiomboleza muda wa majuma matatu kamili.


Naye ataweka hema zake za kifalme kati ya bahari na mlima mtakatifu wa uzuri; lakini ataifikia ajali yake, wala hakuna atakayemsaidia.


Ee Bwana sawasawa na haki yako yote, nakusihi, hasira yako na ghadhabu yako zigeuzwe na kuuacha mji wako Yerusalemu, mlima wako mtakatifu; maana kwa sababu ya dhambi zetu, na maovu ya baba zetu, Yerusalemu na watu wako wamepata kulaumiwa na watu wote wanaotuzunguka.


BWANA asema hivi, Mimi nimerudi Sayuni, nami nitakaa katikati ya Yerusalemu; na Yerusalemu utaitwa, Mji mwaminifu; na mlima wa BWANA wa majeshi utaitwa, mlima mtakatifu.


Hata walipokwisha kumwomba Mungu, mahali pale walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri.


kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;


Maana twajikwaa sisi sote pia katika mambo mengi. Mtu asiyejikwaa katika kunena, huyo ni mtu mkamilifu, awezaye kuuzuia na mwili wake wote kama kwa lijamu.


Akanichukua katika Roho mpaka katika mlima mkubwa, mrefu, akanionesha ule mji mtakatifu, Yerusalemu, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mwenyezi Mungu;


Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo