Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Danieli 8:27 - Swahili Revised Union Version

27 Na mimi, Danieli, nikazimia, nikaugua siku kadhaa; kisha nikaondoka, nikatenda shughuli za mfalme; nami niliyastajabia yale maono, ila hakuna aliyeyafahamu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

27 “Mimi Danieli, nikazimia na kuugua kwa muda. Nilipopona, nikaendelea na shughuli za mfalme. Lakini yale maono yalinistaajabisha, nami sikuweza kuyaelewa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

27 “Mimi Danieli, nikazimia na kuugua kwa muda. Nilipopona, nikaendelea na shughuli za mfalme. Lakini yale maono yalinistaajabisha, nami sikuweza kuyaelewa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

27 “Mimi Danieli, nikazimia na kuugua kwa muda. Nilipopona, nikaendelea na shughuli za mfalme. Lakini yale maono yalinistaajabisha, nami sikuweza kuyaelewa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

27 Mimi Danieli nilikuwa nimechoka sana, na nikalala nikiwa mgonjwa kwa siku kadhaa. Ndipo nikaamka, nikaendelea na shughuli za mfalme. Nilifadhaishwa na maono hayo; sikuweza kuyaelewa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

27 Mimi Danieli nilikuwa nimechoka sana, na nikalala nikiwa mgonjwa kwa siku kadhaa. Ndipo nikaamka, nikaenda kwenye shughuli za mfalme. Nilifadhaishwa na maono hayo, nami sikuweza kuyaelewa.

Tazama sura Nakili

Swahili Roehl Bible 1937

27 Kisha mimi Danieli nikazimia, nikawa mgonjwa siku hizo; kisha nikaondoka kitandani, nikafanya kazi ya kumtumikia mfalame. Lakini nikahangaika sana kwa ajili yao hayo, niliyoyaona, lakini hakuwako aliyenitambua.

Tazama sura Nakili




Danieli 8:27
12 Marejeleo ya Msalaba  

Na kumbe, mmoja mfano wa wanadamu akanigusa midomo yangu; ndipo nikafumbua kinywa changu, nikanena, nikamwambia yeye aliyesimama karibu nami, Ee Bwana wangu, kwa sababu ya maono haya huzuni zangu zimenipata tena; hata sikubakia na nguvu.


Basi nikaachwa peke yangu, nikaona maono haya makubwa, wala hazikubaki nguvu ndani yangu; maana uzuri wangu uligeuzwa ndani yangu kuwa uharibifu, wala sikubakiziwa nguvu.


Ndipo Danieli, aliyeitwa jina lake Belteshaza, akashangaa kwa muda, na fikira zake zikamfadhaisha. Mfalme akajibu akasema, Ee Belteshaza, ndoto ile isikufadhaishe wala tafsiri yake. Belteshaza akajibu, akasema, Bwana wangu, ndoto hii iwapate wao wakuchukiao, na tafsiri yake iwapate adui zako.


Nimesikia habari zako, kwamba roho ya miungu imo ndani yako, na kwamba nuru na ufahamu na akili bora zimeonekana kwako.


Huu ndio mwisho wa jambo lile. Nami, Danieli, fikira zangu zilinifadhaisha, na uso wangu ulinibadilika; lakini nililiweka jambo hilo moyoni mwangu.


Basi alipakaribia mahali niliposimama; nami niliogopa alipokaribia, nikaanguka kifudifudi; lakini aliniambia, Fahamu, Ee mwanadamu, kwa maana maono haya ni ya wakati wa mwisho.


Nami niliona katika maono; nilipokuwa natazama na nikajionea mwenyewe nikiwa huko Susa, Mji mkuu wa mkoa wa Elamu; nikaona katika maono, nami nilikuwa karibu na mto Ulai.


Nikamwona akimkaribia kondoo dume, akamwonea hasira kali, akampiga kondoo dume, akazivunja pembe zake mbili; na huyo kondoo dume alikuwa hana nguvu kusimama mbele yake; bali akamwangusha chini, akamkanyagakanyaga; wala hapakuwapo awezaye kumwokoa kondoo dume katika mkono wake.


Nikasikia, na tumbo langu likatetemeka, Midomo yangu ikatikisika kwa sauti ile; Ubovu ukaingia mifupani mwangu, Nikatetemeka katika mahali pangu; Ili nipate kuingoja ile siku ya dhiki, Kundi lao washambuliao wakweapo juu ya watu.


Naye Samweli akalala hadi asubuhi, akaifungua milango ya nyumba ya BWANA. Samweli akaogopa kumjulisha Eli maono hayo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo