Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Danieli 8:12 - Swahili Revised Union Version

12 Na jeshi likatolewa kwake pamoja na sadaka ya kuteketezwa ya daima, kwa sababu ya makosa; nayo ikaiangusha kweli hata chini; ikatenda ilivyopenda, na kufanikiwa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Viumbe vya mbinguni vikatiwa nguvuni mwake pamoja na tambiko za kuteketezwa kila siku, kwa njia ya upotovu. Nao ukweli ukatupwa chini. Upembe huo ukaibwaga chini ibada ya kweli. Ulifanikiwa katika kila jambo ulilofanya.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Viumbe vya mbinguni vikatiwa nguvuni mwake pamoja na tambiko za kuteketezwa kila siku, kwa njia ya upotovu. Nao ukweli ukatupwa chini. Upembe huo ukaibwaga chini ibada ya kweli. Ulifanikiwa katika kila jambo ulilofanya.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Viumbe vya mbinguni vikatiwa nguvuni mwake pamoja na tambiko za kuteketezwa kila siku, kwa njia ya upotovu. Nao ukweli ukatupwa chini. Upembe huo ukaibwaga chini ibada ya kweli. Ulifanikiwa katika kila jambo ulilofanya.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Kwa sababu ya uasi, jeshi la watakatifu na dhabihu za kila siku vikatiwa mkononi mwake. Pembe hiyo ikafanikiwa katika kila kitu ilichofanya, nayo kweli ikatupwa chini.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Kwa sababu ya uasi, jeshi la watakatifu na dhabihu za kila siku vikatiwa mikononi mwake. Ikafanikiwa katika kila kitu ilichofanya, nayo kweli ikatupwa chini.

Tazama sura Nakili

Swahili Roehl Bible 1937

12 Nacho hicho kikosi kikatolewa pamoja na yale matambiko kwa kupotolewa; nayo mambo ya kweli ikayatupa chini, hivyo yakaendelea iliyoyafanya.

Tazama sura Nakili




Danieli 8:12
14 Marejeleo ya Msalaba  

Hema za wanyang'anyi hufanikiwa, Na hao wamkasirishao Mungu hukaa salama; Mikononi mwao Mungu huleta vitu vingi.


Haki yako ni haki ya milele, Na sheria yako ni kweli.


Usiliondoe neno la kweli kinywani mwangu kamwe, Maana nimezingojea hukumu zako.


Maana hawazifahamu kazi za BWANA, Wala matendo ya mikono yake, Atawavunja wala hatawajenga tena;


Na hukumu imegeuka ikaenda nyuma, na haki inasimama mbali sana; maana kweli imeanguka katika njia kuu, na unyofu hauwezi kuingia.


Wewe u mwenye haki, Ee BWANA, nitetapo nawe, lakini nitasema nawe katika habari ya haki. Mbona njia ya wabaya inasitawi? Mbona wote watendao hila wanakaa salama?


Ndipo atakaporudi mpaka nchi yake mwenye utajiri mwingi; na moyo wake utakuwa kinyume cha hilo agano takatifu; naye atafanya kama apendavyo, na kurudi mpaka nchi yake.


Nikatazama, na pembe iyo hiyo ilifanya vita na watakatifu, ikawashinda;


Nikamwona huyo kondoo dume akisukuma upande wa magharibi, na upande wa kaskazini, na upande wa kusini; wala hakuna mnyama yeyote awezaye kusimama mbele yake, wala hakuna mnyama yeyote awezaye kupokonya mkononi mwake; lakini alitenda kama alivyopenda mwenyewe, akajitukuza nafsi yake.


Tena akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na lugha na taifa.


Naye Daudi alifahamu ya kuwa Sauli amemkusudia mabaya; akamwambia Abiathari, kuhani, Lete hapa hiyo naivera.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo