Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Danieli 6:28 - Swahili Revised Union Version

28 Basi Danieli huyo akafanikiwa katika enzi ya Dario, na katika enzi ya Koreshi, Mwajemi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

28 Basi, Danieli akapata fanaka wakati wa utawala wa mfalme Dario na wa mfalme Koreshi, Mpersi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

28 Basi, Danieli akapata fanaka wakati wa utawala wa mfalme Dario na wa mfalme Koreshi, Mpersi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

28 Basi, Danieli akapata fanaka wakati wa utawala wa mfalme Dario na wa mfalme Koreshi, Mpersi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

28 Hivyo Danieli akastawi wakati wa utawala wa Dario, na utawala wa Koreshi Mwajemi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

28 Hivyo Danieli akastawi wakati wa utawala wa Dario, na utawala wa Koreshi Mwajemi.

Tazama sura Nakili

Swahili Roehl Bible 1937

28 Kisha Danieli akapata kutulia siku za ufalme wa Dario, hata siku za ufalme wa Kiro aliyekuwa Mpersia.

Tazama sura Nakili




Danieli 6:28
10 Marejeleo ya Msalaba  

Ikawa katika mwaka wa kwanza wa Koreshi, mfalme wa Uajemi, ili kwamba neno la BWANA alilolisema kwa kinywa cha Yeremia lipate kutimizwa, BWANA akamwamsha roho yake Koreshi, mfalme wa Uajemi, hata akapiga mbiu katika ufalme wake wote, akaiandika pia, akisema,


Koreshi, mfalme wa Uajemi asema hivi; BWANA, Mungu wa mbinguni, amenipa falme zote za dunia; naye ameniagiza nimjengee nyumba katika Yerusalemu, ulioko Yuda. Basi kila mtu katika ninyi nyote mlio watu wake, BWANA, Mungu wake, na awe pamoja naye, na akwee.


Kwa mkono wako umewakomboa watu wako, Wana wa Yakobo na Yusufu.


nimwambiaye Koreshi, Mchungaji wangu, naye atayatenda mapenzi yangu; hata ataunena Yerusalemu, Utajengwa; na hilo hekalu, Msingi wako utawekwa.


wewe uliyeweka ishara na ajabu katika nchi ya Misri hata siku hii ya leo, katika Israeli na kati ya watu wengine; na kujifanyia jina kama ilivyo leo;


Tena, Danieli huyo akadumu huko hata mwaka wa kwanza wa mfalme Koreshi.


Katika mwaka wa tatu wa Koreshi, mfalme wa Uajemi, Danieli, ambaye jina lake aliitwa Belteshaza, alifunuliwa neno; na neno lile lilikuwa kweli; maana ni vita vikubwa; naye akalifahamu neno lile, akaelewa na maono hayo.


Basi mimi naweka amri ya kuwa kila kabila la watu, na kila taifa, na kila lugha, watakaonena neno lolote lisilopasa juu ya huyo Mungu wa Shadraka, na Meshaki, na Abednego, watakatwa vipande vipande, na nyumba zao zitafanywa jaa; kwa kuwa hakuna Mungu mwingine awezaye kuokoa namna hii.


PERESI, ufalme wako umegawanyika, nao wamepewa Wamedi na Waajemi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo