Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Danieli 6:13 - Swahili Revised Union Version

13 Basi wakajibu, wakasema mbele ya mfalme, Yule Danieli, aliye mmoja wa wana wa wale waliohamishwa wa Yuda, hakujali wewe, Ee mfalme, wala ile marufuku uliyoitia sahihi, bali aomba dua mara tatu kila siku.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Wakamwambia mfalme, “Yule Danieli aliye mmoja wa mateka kutoka nchi ya Yuda hakuheshimu wewe mfalme wala haitii amri uliyotia sahihi. Yeye anasali mara tatu kila siku.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Wakamwambia mfalme, “Yule Danieli aliye mmoja wa mateka kutoka nchi ya Yuda hakuheshimu wewe mfalme wala haitii amri uliyotia sahihi. Yeye anasali mara tatu kila siku.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Wakamwambia mfalme, “Yule Danieli aliye mmoja wa mateka kutoka nchi ya Yuda hakuheshimu wewe mfalme wala haitii amri uliyotia sahihi. Yeye anasali mara tatu kila siku.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Ndipo wakamwambia mfalme, “Danieli, ambaye ni mmoja wa mahamisho kutoka Yuda, hakuheshimu, ee mfalme, wala hajali amri uliyoiweka kwa maandishi. Bado anaomba mara tatu kwa siku.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Ndipo wakamwambia mfalme, “Danieli, ambaye ni mmoja wa mahamisho kutoka Yuda, hakuheshimu, ee mfalme, wala hajali amri uliyoiweka kwa maandishi. Bado anaomba mara tatu kwa siku.”

Tazama sura Nakili

Swahili Roehl Bible 1937

13 Kisha wakamjibu mfalme na kumwambia: Danieli aliye mmoja wao Wayuda waliotekwa na kuhamishwa kuja huku, hakuchi, wala haishiki amri yako, mfalme, ya kutisha watu, uliyoiandika, ila huomba maombo yake kila siku mara tatu.

Tazama sura Nakili

Danieli 6:13
9 Marejeleo ya Msalaba  

Basi Hamani akamwambia mfalme Ahasuero, Kuna watu wa taifa moja waliotawanyika na kukaa kila mahali katikati ya watu wa mataifa walioko katika mikoa yote ya ufalme wako. Nao sheria zao zimetofautiana na sheria za kila taifa; wala hawazishiki amri za mfalme; kwa hiyo haimpasi mfalme kuchukuliana nao.

Basi katika hao walikuwapo baadhi ya wana wa Yuda, Danieli, na Hanania, na Mishaeli, na Azaria.

Ndipo Arioko akamwingiza Danieli mbele ya mfalme kwa haraka, akamwambia hivi, Nimemwona mtu wa hao wana wa Yuda waliohamishwa, atakayemjulisha mfalme ile tafsiri.

na kila mtu asiyeanguka na kuabudu atatupwa katika tanuri liwakalo moto.

Wako Wayahudi kadha wa kadha uliowaweka juu ya mambo ya wilaya ya Babeli, yaani, Shadraka, na Meshaki, na Abednego; watu hawa, Ee mfalme, hawakukujali wewe; hawaitumikii miungu yako, wala kuiabudu ile sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha.

Basi baadhi ya Wakaldayo wakakaribia, wakaleta mashitaka juu ya Wayahudi.

Ndipo Danieli akaletwa mbele ya mfalme. Na Mfalme akanena, akamwambia Danieli, Je! Wewe ndiwe Danieli yule, aliye mmoja wa wana wa Yuda waliohamishwa, ambao mfalme, baba yangu, aliwaleta huku toka Yerusalemu?

na Yasoni amewakaribisha; na hawa wote wanatenda mambo yaliyo kinyume cha amri za Kaisari, wakisema na kusema yupo mfalme mwingine, aitwaye Yesu.

Petro na mitume wakajibu, wakisema, Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo