Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Danieli 5:17 - Swahili Revised Union Version

17 Ndipo Danieli akajibu, akasema mbele ya mfalme; Zawadi zako baki nazo wewe mwenyewe; na thawabu zako mpe mtu mwingine; lakini nitamsomea mfalme maandiko haya, na kumjulisha tafsiri yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Danieli akamjibu mfalme Belshaza, “Waweza kukaa na zawadi zako ee mfalme au kumpa mtu mwingine. Hata hivyo, ee mfalme, nitakusomea maandishi hayo na kukueleza maana yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Danieli akamjibu mfalme Belshaza, “Waweza kukaa na zawadi zako ee mfalme au kumpa mtu mwingine. Hata hivyo, ee mfalme, nitakusomea maandishi hayo na kukueleza maana yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Danieli akamjibu mfalme Belshaza, “Waweza kukaa na zawadi zako ee mfalme au kumpa mtu mwingine. Hata hivyo, ee mfalme, nitakusomea maandishi hayo na kukueleza maana yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Ndipo Danieli akamjibu mfalme, “Unaweza kubaki na zawadi zako mwenyewe na kumpa mtu mwingine thawabu zako. Hata hivyo, nitasoma maandishi kwa mfalme na kumwambia maana yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Ndipo Danieli akamjibu mfalme, “Waweza kubaki na zawadi zako mwenyewe na kumpa mtu mwingine zawadi zako. Hata hivyo, nitasoma maandishi kwa mfalme na kumwambia maana yake.

Tazama sura Nakili

Swahili Roehl Bible 1937

17 Kisha Danieli akamjibu mfalme akisema: Kaa na vipaji vyako! Umpe mwingine matunzo yako! Lakini haya maandiko nitamsomea mfalme, nayo maana yao nitamjulisha.

Tazama sura Nakili




Danieli 5:17
8 Marejeleo ya Msalaba  

ya kuwa sitatwaa uzi wala gidamu ya kiatu wala chochote kilicho chako, usije ukasema, Nimemtajirisha Abramu;


Elisha akamwambia mfalme wa Israeli, Nina nini mimi nawe? Uende kwa manabii wa babayo, na manabii wa mamayo. Mfalme wa Israeli akamwambia, La, sivyo; kwa kuwa BWANA amewakutanisha hawa wafalme watatu, awaue mkononi mwa Moabu.


Lakini akasema, Kama BWANA aishivyo, ambaye nimesimama mbele yake, sipokei kitu. Akamshurutisha apokee; lakini akakataa.


Akamwambia, Je! Moyo wangu haukuenda na wewe, hapo alipogeuka yule mtu katika gari ili akulaki? Je! Huu ndio wakati wa kupokea fedha, na kupokea mavazi, na mashamba ya mizeituni, na mizabibu, na kondoo, na ng'ombe, na watumwa, na wajakazi?


Nitazinena shuhuda zako mbele ya wafalme, Wala sitaona aibu.


Bali kama mkinionesha ile ndoto na tafsiri yake, nitawapa zawadi na thawabu na heshima nyingi; basi nionesheni ile ndoto na tafsiri yake.


Ndipo Belshaza akatoa amri, nao wakamvika Danieli mavazi ya rangi ya zambarau, wakatia mkufu wa dhahabu shingoni mwake, wakapiga mbiu kutangaza habari zake, ya kwamba yeye ni mtu wa tatu katika ufalme.


Lakini Petro akamwambia, Fedha yako na ipotelee mbali pamoja nawe, kwa kuwa umedhania ya kuwa karama ya Mungu yapatikana kwa mali.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo