Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Danieli 4:8 - Swahili Revised Union Version

8 Bali hatimaye Danieli akaingia mbele yangu, ambaye jina lake ni Belteshaza, kwa kufuata jina la mungu wangu; tena ndani yake inakaa roho ya miungu watakatifu; nikamsimulia ile ndoto, nikisema,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Baadaye, akaja Danieli, anayeitwa pia Belteshaza, jina la mungu wangu, ambaye roho ya miungu mitakatifu imo ndani yake. Nami nikamsimulia ndoto yangu, nikasema:

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Baadaye, akaja Danieli, anayeitwa pia Belteshaza, jina la mungu wangu, ambaye roho ya miungu mitakatifu imo ndani yake. Nami nikamsimulia ndoto yangu, nikasema:

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Baadaye, akaja Danieli, anayeitwa pia Belteshaza, jina la mungu wangu, ambaye roho ya miungu mitakatifu imo ndani yake. Nami nikamsimulia ndoto yangu, nikasema:

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Mwishoni, Danieli alikuja mbele yangu, nikamweleza hiyo ndoto. (Danieli anaitwa Belteshaza, kwa jina la mungu wangu, nayo roho ya miungu mitakatifu inakaa ndani yake.)

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Mwishoni, Danieli alikuja mbele yangu nikamweleza hiyo ndoto. (Danieli anaitwa Belteshaza, kwa jina la mungu wangu, nayo roho ya miungu mitakatifu inakaa ndani yake.)

Tazama sura Nakili

Swahili Roehl Bible 1937

8 Mwisho akatokea mbele yangu Danieli aliyeitwa Beltesasari kwa jina la mungu wangu, namo mwake imo roho ya miungu mitakatifu, nikamwambia ndoto nikisema:

Tazama sura Nakili




Danieli 4:8
14 Marejeleo ya Msalaba  

Farao akawaambia watumishi wake, Tupate wapi mtu kama huyu, mwenye Roho ya Mungu ndani yake?


Beli anaanguka chini, Nebo anainama; sanamu zao ziko juu ya wanyama, na juu ya ng'ombe; vitu vile mlivyokuwa mkivichukua huku na huku vimekuwa mzigo, mzigo wa kumlemea mnyama aliyechoka.


Ndipo alipozikumbuka siku za kale, za Musa, na watu wake, akisema, Yuko wapi yeye aliyewapandisha toka baharini pamoja na wachungaji wa kundi lake? Yuko wapi yeye aliyetia kati yao Roho yake Mtakatifu?


Tangazeni katika mataifa, Mkahubiri na kutweka bendera; Hubirini, msifiche, semeni, Babeli umetwaliwa! Beli amefedheheka; Merodaki amefadhaika; Sanamu zake zimeaibishwa, Vinyago vyake vimefadhaika.


juu ya mlima wa mahali palipoinuka pa Israeli nitakipanda; nacho kitatoa matawi, na kuzaa matunda, nao utakuwa mwerezi mzuri; na chini yake watakaa ndege wa kila namna ya mbawa; katika uvuli wa matawi yake watakaa.


Mkuu wa matowashi akawapa majina; alimwita Danieli, Belteshaza; na Hanania akamwita Shadraka; na Mishaeli akamwita Meshaki; na Azaria akamwita Abednego.


Ni neno la ajabu, hili analolitaka mfalme, wala hapana mwingine awezaye kumwonesha mfalme neno hilo, ila miungu, wasio na kikao pamoja na wenye mwili.


Mfalme akajibu, akamwambia Danieli, aliyekuwa akiitwa Belteshaza, Je! Waweza kunijulisha ile ndoto niliyoiona, na tafsiri yake?


Nebukadneza akajibu, akawaambia, Enyi Shadraka, na Meshaki, na Abednego, je! Ni kwa makusudi hata hamumtumikii mungu wangu wala kuisujudia sanamu ya dhahabu niliyoisimamisha?


Mimi, Nebukadneza, nimeiona ndoto hii; na wewe, Ee Belteshaza, eleza tafsiri yake, kwa maana wenye hekima wote wa ufalme wangu hawawezi kunijulisha tafsiri yake; bali wewe waweza, maana roho ya miungu watakatifu inakaa ndani yako.


Ee Belteshaza, mkuu wa waaguzi, kwa sababu ninajua ya kuwa roho ya miungu watakatifu inakaa ndani yako, na ya kuwa hapana neno la siri likushindalo, niambie maana ya hii ndoto yangu niliyoiona, na tafsiri yake.


Nimesikia habari zako, kwamba roho ya miungu imo ndani yako, na kwamba nuru na ufahamu na akili bora zimeonekana kwako.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo