Danieli 4:16 - Swahili Revised Union Version16 moyo wake ubadilike, usiwe moyo wa binadamu, na apewe moyo wa mnyama; nyakati saba zikapite juu yake. Tazama suraMatoleo zaidiBiblia Habari Njema16 Akili yake ya utu ibadilishwe, awe na akili ya mnyama kwa miaka saba. Tazama suraBiblia Habari Njema - BHND16 Akili yake ya utu ibadilishwe, awe na akili ya mnyama kwa miaka saba. Tazama suraBiblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza16 Akili yake ya utu ibadilishwe, awe na akili ya mnyama kwa miaka saba. Tazama suraNeno: Bibilia Takatifu16 Akili yake na ibadilishwe kutoka ile ya mwanadamu, na apewe akili ya mnyama, hadi nyakati saba zipite juu yake. Tazama suraNeno: Maandiko Matakatifu16 Akili yake na ibadilishwe kutoka ile ya mwanadamu na apewe akili ya mnyama, mpaka nyakati saba zipite juu yake. Tazama suraSwahili Roehl Bible 193716 Moyo wake utageuzwa, usiwe wa kimtu tena, apewe moyo wa kinyama, mpaka miaka saba ipite, akiwa hivyo. Tazama sura |
Nami nikamsikia yule mtu aliyevikwa nguo za kitani, aliyekuwa juu ya maji ya mto, hapo alipoinua mkono wake wa kulia na mkono wake wa kushoto kuelekea mbinguni; akaapa kwa yeye aliye hai milele na milele, ya kwamba itakuwa nyakati tatu na nusu; tena watakapokuwa wamekwisha kuvunja nguvu za hao watu watakatifu, ndipo mambo hayo yote yatakapotimizwa.
Tena, kwa kuwa mfalme alimwona mlinzi, naye ni mtakatifu, akishuka kutoka mbinguni, akisema, Ukateni mti huu, mkauangamize; ila kiacheni kisiki cha shina lake katika ardhi, pamoja na pingu ya chuma na shaba, katika majani mororo ya kondeni; kikatiwe maji kwa umande wa mbinguni, na sehemu yake iwe pamoja na wanyama wa mwituni, hata nyakati saba zipite juu yake;
ya kuwa utafukuzwa mbali na wanadamu, na makao yako yatakuwa pamoja na wanyama wa mwituni, nawe utalazimishwa kula majani kama ng'ombe, nawe utanyeshewa na umande wa mbinguni, na nyakati saba zitapita juu yako; hata utakapojua ya kuwa Aliye Juu ndiye anayemiliki katika ufalme wa wanadamu, naye humpa yeye amtakaye, awaye yote.