Danieli 4:13 - Swahili Revised Union Version13 Nikaona katika njozi za kichwa changu kitandani mwangu, na tazama, mlinzi, naye ni mtakatifu, alishuka kutoka mbinguni. Tazama suraMatoleo zaidiBiblia Habari Njema13 “Nilipokuwa nimelala kitandani, niliona maono: Mlinzi mtakatifu alishuka kutoka mbinguni. Tazama suraBiblia Habari Njema - BHND13 “Nilipokuwa nimelala kitandani, niliona maono: Mlinzi mtakatifu alishuka kutoka mbinguni. Tazama suraBiblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza13 “Nilipokuwa nimelala kitandani, niliona maono: Mlinzi mtakatifu alishuka kutoka mbinguni. Tazama suraNeno: Bibilia Takatifu13 “Katika maono niliyoyaona nikiwa nimelala kitandani mwangu, nilitazama, na mbele yangu nikaona mlinzi, aliye mtakatifu, akishuka kutoka mbinguni. Tazama suraNeno: Maandiko Matakatifu13 “Katika maono niliyoyaona nikiwa nimelala kitandani mwangu, nilitazama, na mbele yangu alikuwepo mlinzi, aliye mtakatifu, akishuka kutoka mbinguni. Tazama suraSwahili Roehl Bible 193713 Nilipokuwa ninautazama katika maono, niliyoyaona kwa macho yangu nilipolala kitandani, mara nikaona, mlinzi mtakatifu akishuka kutoka mbinguni. Tazama sura |
Tena, kwa kuwa mfalme alimwona mlinzi, naye ni mtakatifu, akishuka kutoka mbinguni, akisema, Ukateni mti huu, mkauangamize; ila kiacheni kisiki cha shina lake katika ardhi, pamoja na pingu ya chuma na shaba, katika majani mororo ya kondeni; kikatiwe maji kwa umande wa mbinguni, na sehemu yake iwe pamoja na wanyama wa mwituni, hata nyakati saba zipite juu yake;