Danieli 3:7 - Swahili Revised Union Version7 Basi wakati huo, watu wa kabila zote walipoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zumari, na namna zote za ngoma, watu wote na mataifa na lugha wakaanguka, wakaiabudu ile sanamu, mfalme Nebukadneza aliyoisimamisha. Tazama suraMatoleo zaidiBiblia Habari Njema7 Kwa hiyo, watu wote, mara waliposikia sauti za baragumu, filimbi, kinubi, zeze, santuri, zumari na sauti za ala nyingine za muziki, walianguka kifudifudi na kuiabudu ile sanamu ya dhahabu ambayo mfalme Nebukadneza aliisimamisha. Tazama suraBiblia Habari Njema - BHND7 Kwa hiyo, watu wote, mara waliposikia sauti za baragumu, filimbi, kinubi, zeze, santuri, zumari na sauti za ala nyingine za muziki, walianguka kifudifudi na kuiabudu ile sanamu ya dhahabu ambayo mfalme Nebukadneza aliisimamisha. Tazama suraBiblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza7 Kwa hiyo, watu wote, mara waliposikia sauti za baragumu, filimbi, kinubi, zeze, santuri, zumari na sauti za ala nyingine za muziki, walianguka kifudifudi na kuiabudu ile sanamu ya dhahabu ambayo mfalme Nebukadneza aliisimamisha. Tazama suraNeno: Bibilia Takatifu7 Kwa hiyo, mara waliposikia sauti ya baragumu, filimbi, marimba, zeze, kinubi, zumari, na aina zote za sauti za ala za uimbaji, watu wa makabila yote, na mataifa, na wa kila lugha wakasujudu na kuiabudu ile sanamu ya dhahabu ambayo Mfalme Nebukadneza alikuwa ameisimamisha. Tazama suraNeno: Maandiko Matakatifu7 Kwa hiyo, mara waliposikia sauti ya baragumu, filimbi, kinubi, zeze, kinanda na aina zote za ala za uimbaji, watu wa kabila zote, mataifa na watu wa kila lugha wakaanguka chini na kuiabudu ile sanamu ya dhahabu ambayo Mfalme Nebukadneza alikuwa ameisimamisha. Tazama suraSwahili Roehl Bible 19377 Kwa sababu hii siku ile ilipofika, wao wote wa makabila ya watu walipozisikia sauti za mabaragumu na za filimbi na za marimba na za mapango na za mazeze na za namna zote za ngoma, basi, ndipo, makabila na koo zote za watu, wao wote wenye ndimi za watu walipoanguka wakikisujudia hicho kinyago cha dhahabu, mfalme Nebukadinesari alichokisimamisha. Tazama sura |
Yule mnyama uliyemwona alikuwako, naye hayuko, naye yuko tayari kupanda kutoka kuzimu na kwenda kwenye uharibifu. Na hao wakaao juu ya nchi, wasioandikwa majina yao katika kitabu cha uzima tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, watastaajabu wamwonapo yule mnyama, ya kwamba alikuwako, naye hayuko, naye atakuwako.