Danieli 3:3 - Swahili Revised Union Version3 Ndipo maamiri, wasimamizi, watawala, washauri, watunza hazina, majaji, mahakimu na wakuu wa wilaya zote, wakakusanyika ili kuizindua ile sanamu, mfalme Nebukadneza aliyoisimamisha; wakasimama mbele ya ile sanamu, mfalme Nebukadneza aliyoisimamisha. Tazama suraMatoleo zaidiBiblia Habari Njema3 Basi, maliwali, wasimamizi, wakuu wa mikoa, washauri, watunza hazina, majaji, mahakimu na maofisa wote wa mikoa wakakusanyika tayari kwa uzinduzi wa sanamu aliyosimamisha mfalme Nebukadneza. Tazama suraBiblia Habari Njema - BHND3 Basi, maliwali, wasimamizi, wakuu wa mikoa, washauri, watunza hazina, majaji, mahakimu na maofisa wote wa mikoa wakakusanyika tayari kwa uzinduzi wa sanamu aliyosimamisha mfalme Nebukadneza. Tazama suraBiblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza3 Basi, maliwali, wasimamizi, wakuu wa mikoa, washauri, watunza hazina, majaji, mahakimu na maofisa wote wa mikoa wakakusanyika tayari kwa uzinduzi wa sanamu aliyosimamisha mfalme Nebukadneza. Tazama suraNeno: Bibilia Takatifu3 Basi wakuu, wasimamizi, watawala, washauri, watunza hazina, waamuzi, mahakimu, na maafisa wengine wote wa jimbo wakakusanyika ili kuizindua sanamu ile Mfalme Nebukadneza alikuwa ameisimamisha, nao wakasimama mbele ya hiyo sanamu. Tazama suraNeno: Maandiko Matakatifu3 Basi wakuu, wasimamizi, watawala, washauri, watunza hazina, waamuzi, mahakimu na maafisa wengine wa jimbo walikusanyika ili kuizindua sanamu ile Mfalme Nebukadneza alikuwa ameisimamisha, nao wakasimama mbele ya hiyo sanamu. Tazama suraSwahili Roehl Bible 19373 Ndipo, walipokusanyika wenye amri na wakuu na watawala nchi na waamuzi na watunza mali na mabwana shauri na wandewa na wakuu wote wa nchi kukieua kinyago hicho, mfalme Nebukadinesari alichokisimamisha, wakasimama mbele ya hicho kinyago, Nebukadinesari alichokisimamisha. Tazama sura |