Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Danieli 2:46 - Swahili Revised Union Version

46 Ndipo Nebukadneza, mfalme, akaanguka kifudifudi, akamsujudia Danieli, akatoa amri wamtolee Danieli sadaka na uvumba.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

46 Ndipo mfalme Nebukadneza alipoanguka kifudifudi na kumsujudia Danieli na kuamuru wamtolee Danieli tambiko na ubani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

46 Ndipo mfalme Nebukadneza alipoanguka kifudifudi na kumsujudia Danieli na kuamuru wamtolee Danieli tambiko na ubani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

46 Ndipo mfalme Nebukadneza alipoanguka kifudifudi na kumsujudia Danieli na kuamuru wamtolee Danieli tambiko na ubani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

46 Ndipo Mfalme Nebukadneza akaanguka kifudifudi mbele ya Danieli kumpa heshima, akaagiza wamtolee Danieli sadaka na uvumba.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

46 Ndipo Mfalme Nebukadneza akaanguka kifudifudi mbele ya Danieli kumpa heshima, akaagiza wamtolee Danieli sadaka na uvumba.

Tazama sura Nakili

Swahili Roehl Bible 1937

46 Ndipo, mfalme Nebukadinesari alipoanguka kifudifudi, kisha akamwinamia Danieli, akaagiza kumtolea vipaji vya tambiko na uvumba.

Tazama sura Nakili




Danieli 2:46
12 Marejeleo ya Msalaba  

wapate kumtolea Mungu wa mbinguni sadaka zenye harufu nzuri, na kumwombea mfalme, na wanawe, wapate uzima.


wakati mtakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zumari, na namna zote za ngoma, lazima kuanguka na kuiabudu sanamu ya dhahabu, mfalme Nebukadneza aliyoisimamisha.


Basi wakati huo, watu wa kabila zote walipoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zumari, na namna zote za ngoma, watu wote na mataifa na lugha wakaanguka, wakaiabudu ile sanamu, mfalme Nebukadneza aliyoisimamisha.


Basi alipakaribia mahali niliposimama; nami niliogopa alipokaribia, nikaanguka kifudifudi; lakini aliniambia, Fahamu, Ee mwanadamu, kwa maana maono haya ni ya wakati wa mwisho.


Nami nitaifanya miji yenu iwe maganjo, na mahali penu patakatifu nitapatia ukiwa; wala sitasikia harufu ya manukato yenu yapendezayo.


akaanguka kifudifudi miguuni pake, akamshukuru; naye alikuwa Msamaria.


Petro alipokuwa akiingia Kornelio akatoka amlaki akamwangukia miguuni mwake, akamsujudia.


Kuhani wa Zeu ambaye hekalu lake lilikuwa mbele ya mji, akaleta ng'ombe na mataji ya maua hadi malangoni, akitaka kutoa dhabihu pamoja na umati wa watu.


Wao wakadhani ya kuwa atavimba au kuanguka chini kwa kufa ghafla; na wakiisha kumwangalia sana, na kuona kwamba halimpati dhara lolote, wakageuka, wakasema kwamba yeye ni mungu.


Na wale wazee ishirini na wanne waketio mbele za Mungu katika viti vya enzi vyao wakaanguka kifudifudi, wakamsujudia Mungu


Nami nikaanguka mbele ya miguu yake, ili nimsujudie; akaniambia, Angalia, usifanye hivi; mimi ni mtumishi mwenzako na wa ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Msujudie Mungu. Kwa maana ushuhuda wa Yesu ndio roho ya unabii.


Nami Yohana ndimi niliyeyasikia na kuyaona mambo hayo. Na hapo nilipoyasikia na kuyaona nilianguka, ili nisujudu mbele ya miguu ya malaika yule mwenye kunionesha hayo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo