Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Danieli 11:41 - Swahili Revised Union Version

41 Tena ataingia katika hiyo nchi ya uzuri, na nchi nyingi zitapinduliwa; lakini nchi hizi zitaokolewa na mkono wake, Edomu, na Moabu, na wakuu wa watu wa Amoni.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

41 Ataivamia hata nchi ile tukufu na kuua maelfu ya watu. Lakini nchi za Edomu, Moabu na sehemu kubwa ya Amoni, zitaokoka kutoka mikononi mwake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

41 Ataivamia hata nchi ile tukufu na kuua maelfu ya watu. Lakini nchi za Edomu, Moabu na sehemu kubwa ya Amoni, zitaokoka kutoka mikononi mwake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

41 Ataivamia hata nchi ile tukufu na kuua maelfu ya watu. Lakini nchi za Edomu, Moabu na sehemu kubwa ya Amoni, zitaokoka kutoka mikononi mwake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

41 Pia ataivamia Nchi ya Kupendeza. Nchi nyingi zitapinduliwa, bali Edomu, Moabu, na viongozi wa Amoni wataokolewa kutoka mkono wake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

41 Pia ataivamia Nchi ya Kupendeza. Nchi nyingi zitapinduliwa, bali Edomu, Moabu na viongozi wa Amoni wataokolewa kutoka mkono wake.

Tazama sura Nakili

Swahili Roehl Bible 1937

41 Kisha ataiingia nayo hiyo nchi yenye utukufu; ndipo, nchi nyingi zitakapoangamizwa; zitakazopona mikoni mwake ni za Edomu na za Moabu na wakuu wao wana wa Amoni.

Tazama sura Nakili




Danieli 11:41
9 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini nitawarudisha watu wa Moabu walio utumwani, siku za mwisho, asema BWANA. Hukumu ya Moabu imefikia hapa.


Lakini baada ya hayo nitawarudisha wana wa Amoni walio utumwani, asema BWANA.


Misri, na Yuda, na Edomu, na wana wa Amoni, na Moabu, na wote wenye kunyoa denge, wakaao nyikani; maana mataifa hayo yote hawana tohara, wala nyumba yote ya Israeli hawakutahiriwa mioyo yao.


Maana ajaye kupigana naye atatenda kadiri apendavyo, wala hapana mtu atakayesimama mbele yake; naye atasimama katika nchi ya uzuri, na uharibifu utakuwa mkononi mwake.


Naye ataunyosha mkono wake juu ya nchi hizo, hata na nchi ya Misri haitaokoka.


Naye ataweka hema zake za kifalme kati ya bahari na mlima mtakatifu wa uzuri; lakini ataifikia ajali yake, wala hakuna atakayemsaidia.


Na katika moja ya pembe hizo ilitokea pembe ndogo, iliyokua sana, upande wa kusini, na upande wa magharibi, na upande wa nchi ya uzuri.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo