Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Danieli 11:39 - Swahili Revised Union Version

39 Naye ataziteka nyara ngome zenye nguvu kwa msaada wa mungu mgeni; na yeye atakayemkubali atamwongeza kwa utukufu; naye atawapa kumiliki wengi; naye ataigawa nchi kwa rushwa.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

39 Atazishughulikia ngome zake kwa msaada wa mungu wa kigeni. Wale wanaomtambua kuwa mfalme, atawatunukia heshima kubwa, atawapa vyeo vikubwa na kuwagawia ardhi kama zawadi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

39 Atazishughulikia ngome zake kwa msaada wa mungu wa kigeni. Wale wanaomtambua kuwa mfalme, atawatunukia heshima kubwa, atawapa vyeo vikubwa na kuwagawia ardhi kama zawadi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

39 Atazishughulikia ngome zake kwa msaada wa mungu wa kigeni. Wale wanaomtambua kuwa mfalme, atawatunukia heshima kubwa, atawapa vyeo vikubwa na kuwagawia ardhi kama zawadi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

39 Atashambulia ngome zenye nguvu mno kwa msaada wa mungu wa kigeni, naye atawaheshimu sana wale watakaomkubali yeye. Atawafanya watawala wa watu wengi, na atagawa nchi kwa gharama.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

39 Atashambulia ngome zenye nguvu mno kwa msaada wa mungu wa kigeni naye atawaheshimu sana wale watakaomkubali yeye. Atawafanya watawala juu ya watu wengi, na atagawa nchi kwa gharama.

Tazama sura Nakili

Swahili Roehl Bible 1937

39 Katika miji yenye maboma atafanya hivyo kwa ajili ya huyo mungu mgeni: atakayemwungama atampa macheo mengi, tena atampa watu wengi kuwatawala, nayo nchi atamgawia kuwa malipo yake.

Tazama sura Nakili

Danieli 11:39
3 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini katika mahali pake atamheshimu mungu wa ngome; na mungu ambaye baba zake hawakumjua atamheshimu, kwa dhahabu, na fedha, na vito vya thamani, na vitu vipendezavyo.

Na wakati wa mwisho mfalme wa kusini atashindana naye; na mfalme wa kaskazini atamshambulia kama upepo wa kisulisuli, pamoja na magari ya vita, na wapanda farasi, na merikebu nyingi; naye ataingia katika nchi hizo, na kufurika na kupita katikati.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo