Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Danieli 11:20 - Swahili Revised Union Version

20 Ndipo badala yake atasimama mmoja, atakayepitisha mwenye kutoza ushuru kati ya utukufu wa ufalme wake; lakini katika muda wa siku chache ataangamizwa, si kwa hasira, wala si katika vita.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

20 “ ‘Huyu atafuatwa na mfalme mwingine ambaye atatuma mtozaushuru kupitia katika fahari ya ufalme wake. Mfalme huyo atauawa baada ya siku chache, lakini si kwa hasira wala vitani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

20 “ ‘Huyu atafuatwa na mfalme mwingine ambaye atatuma mtozaushuru kupitia katika fahari ya ufalme wake. Mfalme huyo atauawa baada ya siku chache, lakini si kwa hasira wala vitani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

20 “‘Huyu atafuatwa na mfalme mwingine ambaye atatuma mtozaushuru kupitia katika fahari ya ufalme wake. Mfalme huyo atauawa baada ya siku chache, lakini si kwa hasira wala vitani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

20 “Atakayetawala baada yake atamtuma mtoza ushuru ili kudumisha fahari ya kifalme. Hata hivyo, baada ya miaka michache ataangamizwa, lakini si katika hasira wala katika vita.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

20 “Atakayetawala baada yake atamtuma mtoza ushuru ili kudumisha fahari ya kifalme. Hata hivyo, baada ya miaka michache ataangamizwa, lakini si katika hasira wala katika vita.

Tazama sura Nakili

Swahili Roehl Bible 1937

20 Mahali pake ataondokea mwingine atakayetuma mtoza kodi penye utukufu wa ufalme wake; lakini kwa muda wa siku chache atavunjwa, lakini haitakuwa kwa ukali wa mtu wala kwa mapigano.

Tazama sura Nakili




Danieli 11:20
7 Marejeleo ya Msalaba  

Na Yehoyakimu akampa Farao dhahabu na fedha; lakini akaitoza nchi kodi, ili apate kutoa zile fedha kwa amri yake Farao; akawatoza fedha na dhahabu watu wa nchi, kila mtu kwa kodi yake, ili ampe Farao Neko.


Kwa maana kupiga maziwa huleta siagi; Na kupiga pua hutokeza damu; kadhalika kuchochea hasira hutokeza ugomvi.


Badala ya shaba nitaleta dhahabu, Na badala; ya chuma nitaleta fedha, Na badala ya mti, shaba, Na badala ya mawe, chuma; Tena nitaifanya amani kuwa kama msimamizi wako, Na haki kuwa kiongozi wako.


Kisha badala yake atasimama mmoja, mtu astahiliye kudharauliwa, ambaye hawakumpa heshima ya ufalme; naye atakuja wakati wa amani, naye ataupata ufalme kwa kujipendekeza.


Lakini katika chipukizi la mizizi yake atasimama mmoja mahali pake atakayeliendesha jeshi la askari, naye ataingia katika ngome ya mfalme wa kaskazini, na kuwatenda mambo, na kuwashinda;


Ufunuo aliouona nabii Habakuki.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo