Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Danieli 10:20 - Swahili Revised Union Version

20 Ndipo akasema, Je! Unajua sababu iliyonileta kwako? Na sasa nitarudi ili nipigane na mkuu wa Uajemi; nami nitakapotoka huku, tazama, mkuu wa Ugiriki atakuja.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

20 Naye akaniambia, ‘Je, unajua kwa nini nimekujia? Sasa ni lazima nirudi kupigana na malaika mlinzi wa Persia. Halafu, nitakapokuwa nimemshinda, malaika mlinzi wa mfalme wa Ugiriki atatokea.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

20 Naye akaniambia, ‘Je, unajua kwa nini nimekujia? Sasa ni lazima nirudi kupigana na malaika mlinzi wa Persia. Halafu, nitakapokuwa nimemshinda, malaika mlinzi wa mfalme wa Ugiriki atatokea.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

20 Naye akaniambia, ‘Je, unajua kwa nini nimekujia? Sasa ni lazima nirudi kupigana na malaika mlinzi wa Persia. Halafu, nitakapokuwa nimemshinda, malaika mlinzi wa mfalme wa Ugiriki atatokea.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

20 Kwa hiyo akasema, “Je, unajua kwa nini nimekujia? Sasa hivi nitarudi kupigana dhidi ya mkuu wa Uajemi, nami nikienda, mkuu wa Uyunani atakuja.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

20 Kwa hiyo akasema, “Je, unajua kwa nini nimekujia? Sasa hivi nitarudi kupigana dhidi ya mkuu wa Uajemi, nami nikienda, mkuu wa Uyunani atakuja.

Tazama sura Nakili

Swahili Roehl Bible 1937

20 Akauliza: Unajua, kama ni kwa sababu gani, nikikujia? Sasa nitarudi kupigana naye mkuu wa Persia. Hapo, nitakapotoka kwake, papo hapo atakuja mkuu wa Ugriki.

Tazama sura Nakili

Danieli 10:20
8 Marejeleo ya Msalaba  

Ndipo wakazi wa nchi wakawavunja moyo watu wa Yuda, wakawafanya wawe na hofu ya kujenga.

Basi malaika wa BWANA alitoka, akaua watu elfu mia moja na themanini na tano katika kituo cha Waashuri, na watu walipoamka asubuhi na mapema, kumbe, hao walikuwa maiti wote pia.

Lakini mkuu wa ufalme wa Uajemi alinipinga siku ishirini na moja; bali, tazama, huyo Mikaeli, mmoja wa hao wakuu wa mbele, akaja kunisaidia; nami nikamwacha huko pamoja na wafalme wa Uajemi.

Kisha nikatazama, na kumbe! Mnyama mwingine, kama chui, naye juu ya mgongo wake alikuwa na mabawa manne kama ya ndege; mnyama huyo alikuwa na vichwa vinne; akapewa mamlaka.

Na yule beberu, mwenye manyoya mengi, ni mfalme wa Ugiriki; na ile pembe kubwa iliyo kati ya macho yake ni mfalme wa kwanza.

Mara malaika wa Bwana akampiga, kwa sababu hakumpa Mungu utukufu; akaliwa na wadudu, akatokwa na roho.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo