Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Amosi 6:14 - Swahili Revised Union Version

14 Maana, angalia, nitaleta taifa juu yenu, enyi nyumba ya Israeli, asema BWANA, Mungu wa majeshi, nao watawatesa ninyi toka mahali pa kuingilia katika Hamathi hata kijito cha Araba.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: “Enyi Waisraeli, kweli nitaleta taifa moja lije kuwashambulia, nalo litawatesa nyinyi kuanzia Lebo-hamathi kaskazini, hadi kijito cha Araba, upande wa kusini.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: “Enyi Waisraeli, kweli nitaleta taifa moja lije kuwashambulia, nalo litawatesa nyinyi kuanzia Lebo-hamathi kaskazini, hadi kijito cha Araba, upande wa kusini.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: “Enyi Waisraeli, kweli nitaleta taifa moja lije kuwashambulia, nalo litawatesa nyinyi kuanzia Lebo-hamathi kaskazini, hadi kijito cha Araba, upande wa kusini.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Maana Bwana Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, asema, “Nitainua taifa dhidi yenu, ee nyumba ya Israeli, nalo litawatesa kuanzia Lebo-Hamathi hadi Bonde la Araba.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Maana bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote asema, “Nitainua taifa dhidi yenu, ee nyumba ya Israeli, nalo litawatesa kuanzia Lebo-Hamathi hadi Bonde la Araba.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

14 Maana, angalia, nitaleta taifa juu yenu, enyi nyumba ya Israeli, asema BWANA, Mungu wa majeshi, nao watawatesa ninyi toka mahali pa kuingilia katika Hamathi hata kijito cha Araba.

Tazama sura Nakili

Amosi 6:14
13 Marejeleo ya Msalaba  

Basi, wakati ule Sulemani akafanya sikukuu, na Israeli wote pamoja naye, kusanyiko kubwa sana, kutoka maingilio ya Hamathi mpaka kijito cha Misri, mbele za BWANA, Mungu wetu, siku saba na siku saba, yaani siku kumi na nne.

Yeye akaurudisha mpaka wa Israeli toka kuingia kwa Hamathi hata bahari ya Araba, sawasawa na neno la BWANA, Mungu wa Israeli, alilolinena kwa mkono wa mtumishi wake Yona mwana wa Amitai, nabii, aliyekuwa wa Gath-heferi.

Katika siku za Peka mfalme wa Israeli akaja Tiglath-pileseri mfalme wa Ashuru, akatwaa Iyoni, na Abel-beth-maaka, na Yanoa, na Kedeshi, na Hazori, na Gileadi, na Galilaya, nchi yote ya Naftali; akawahamisha hao watu mpaka Ashuru.

Katika mwaka wa tisa wa Hoshea, huyo mfalme wa Ashuru akautwaa Samaria, akawahamisha Israeli mpaka Ashuru, akawaweka katika Hala na Habori, karibu na mto wa Gozani, na katika miji ya Wamedi.

Katika siku hiyo Bwana atanyoa kichwa na malaika ya miguuni, kwa wembe ulioajiriwa pande za ng'ambo ya Mto, yaani, kwa mfalme wa Ashuru, nao utaziondoa ndevu pia.

Na upande wa magharibi, utakuwa ni bahari kubwa, kutoka mpaka wa kusini mpaka mahali penye kuelekea maingilio ya Hamathi. Huu ndio upande wa magharibi.

Wakaao Samaria wataona hofu kwa ajili ya ndama za Beth-aveni; kwa maana watu wa mji huo wataulilia, na makuhani wake walioufurahia, kwa sababu ya utukufu wake; kwa maana umetoweka.

Basi, haya ndiyo asemayo Bwana MUNGU; Atakuwako adui, kuizunguka nchi pande zote; naye atazishusha chini nguvu zako zikutoke; na majumba yako yatatekwa nyara.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo