Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Amosi 3:11 - Swahili Revised Union Version

11 Basi, haya ndiyo asemayo Bwana MUNGU; Atakuwako adui, kuizunguka nchi pande zote; naye atazishusha chini nguvu zako zikutoke; na majumba yako yatatekwa nyara.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Kwa hiyo, adui ataizingira nchi yao, atapaharibu mahali pao pa kujihami, na kuziteka nyara ikulu zao.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Kwa hiyo, adui ataizingira nchi yao, atapaharibu mahali pao pa kujihami, na kuziteka nyara ikulu zao.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Kwa hiyo, adui ataizingira nchi yao, atapaharibu mahali pao pa kujihami, na kuziteka nyara ikulu zao.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: “Adui ataizingira nchi; ataangusha chini ngome zenu na kuteka nyara maboma yenu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Kwa hiyo hili ndilo asemalo bwana Mwenyezi: “Adui ataizingira nchi; ataangusha chini ngome zenu na kuteka nyara maboma yenu.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

11 Basi, haya ndiyo asemayo Bwana MUNGU; Atakuwako adui, kuizunguka nchi pande zote; naye atazishusha chini nguvu zako zikutoke; na majumba yako yatatekwa nyara.

Tazama sura Nakili




Amosi 3:11
17 Marejeleo ya Msalaba  

Wana wa Yakobo wakawajia hao waliouawa, wakaupora mji kwa sababu wamemharibu dada yao.


Akaja Pulu mfalme wa Ashuru juu ya nchi; naye Menahemu akampa Pulu talanta elfu moja za fedha, ili kwamba mkono wake uwe pamoja naye, na ufalme uwe imara mkononi mwake.


Katika siku za Peka mfalme wa Israeli akaja Tiglath-pileseri mfalme wa Ashuru, akatwaa Iyoni, na Abel-beth-maaka, na Yanoa, na Kedeshi, na Hazori, na Gileadi, na Galilaya, nchi yote ya Naftali; akawahamisha hao watu mpaka Ashuru.


Wakaiteketeza nyumba ya Mungu, wakaubomoa ukuta wa Yerusalemu, wakayateketeza kwa moto majumba yake yote, wakaviharibu vyombo vyake vyote vya thamani.


Hakikusalia kitu asichokula; Kwa hiyo kufanikiwa kwake hakutadumu.


lakini nitatuma moto juu ya Yuda, nao utayateketeza majumba ya Yerusalemu. Hukumu kwa Israeli.


Kwa maana hawajui kutenda haki, asema BWANA, hao wawekao akiba ya jeuri na unyang'anyi katika majumba yao.


Nami nitaipiga nyumba ya wakati wa baridi pamoja na nyumba ya wakati wa joto; na hizo nyumba za pembe zitaangamia, nazo nyumba kubwa zitakuwa na mwisho, asema BWANA.


Maana, angalia, nitaleta taifa juu yenu, enyi nyumba ya Israeli, asema BWANA, Mungu wa majeshi, nao watawatesa ninyi toka mahali pa kuingilia katika Hamathi hata kijito cha Araba.


Bwana MUNGU ameapa kwa nafsi yake, asema BWANA, Mungu wa majeshi; Naizira fahari ya Yakobo, nachukizwa na majumba yake; kwa sababu hiyo nitautoa huo mji, pamoja na wote waliomo ndani yake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo