Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




2 Wakorintho 10:8 - Swahili Revised Union Version

8 Maana, nijapojisifu zaidi kidogo kwa ajili ya mamlaka yetu, (tuliyopewa na Bwana, tupate kuwajenga wala si kuwaangusha), sitatahayarika;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Hata kama nimezidi katika kujivuna kwangu juu ya ule uwezo aliotupa – uwezo wa kuwajenga na sio wa kubomoa – hata hivyo sijuti hata kidogo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Hata kama nimezidi katika kujivuna kwangu juu ya ule uwezo aliotupa – uwezo wa kuwajenga na sio wa kubomoa – hata hivyo sijuti hata kidogo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Hata kama nimezidi katika kujivuna kwangu juu ya ule uwezo aliotupa — uwezo wa kuwajenga na sio wa kubomoa — hata hivyo sijuti hata kidogo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Basi hata nikijisifu zaidi kidogo kuhusu mamlaka tuliyo nayo, ambayo Bwana Isa alitupatia ili kuwajenga wala si kuwabomoa, mimi sitaionea haya.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Basi hata kama nikijisifu zaidi kidogo kuhusu mamlaka tuliyo nayo, ambayo Bwana Isa alitupa ili kuwajenga wala si kuwabomoa, mimi sitaionea haya.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

8 Maana, nijapojisifu zaidi kidogo kwa ajili ya mamlaka yetu, (tuliyopewa na Bwana, tupate kuwajenga wala si kuwaangusha), sitatahayarika;

Tazama sura Nakili




2 Wakorintho 10:8
12 Marejeleo ya Msalaba  

Si kwamba tunatawala imani yenu; bali tu wasaidizi wa furaha yenu; maana kwa imani yenu mnasimama.


(maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;)


nisije nikaonekana kana kwamba nataka kuwaogofya kwa nyaraka zangu.


Mnadhani hata sasa ya kuwa najitetea kwenu! Mbele za Mungu twanena katika Kristo. Na hayo yote, wapenzi, ni kwa ajili ya kuwajenga ninyi.


Maana kama ningetaka kujisifu singekuwa mpumbavu, kwa sababu nitasema kweli. Lakini najizuia, ili mtu asinihesabie zaidi ya hayo ayaonayo kwangu au kuyasikia kwangu.


Kwa sababu hiyo, naandika haya nikiwa mbali nanyi, ili, nikija, nisiwe na ukali wa kadiri ya uwezo ule niliopewa na Bwana, kwa kujenga wala si kwa kubomoa.


Maana hatuwezi kutenda neno lolote kinyume cha kweli, bali kwa ajili ya kweli.


Kwa maana, ikiwa nimejisifu mbele yake katika neno lolote kwa ajili yenu, sikutahayarishwa; bali, kama tulivyowaambia mambo yote kwa kweli, vivyo hivyo na kujisifu kwetu kwa Tito kulikuwa kweli.


Ninao ujasiri mwingi kwenu; naona fahari kuu juu yenu. Nimejaa faraja, katika dhiki yetu yote nimejaa furaha ya kupita kiasi.


Paulo, mtume, (si mtume wa wanadamu, wala kutumwa na mwanadamu, bali na Yesu Kristo, na Mungu Baba aliyemfufua kutoka kwa wafu),


Kwa sababu hiyo nimepatikana na mateso haya, lakini sitahayari; kwa maana namjua yeye niliyemwamini, na kusadiki ya kwamba aweza kukilinda kile nilichokiweka amana kwake hata siku ile.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo