Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




2 Wafalme 21:9 - Swahili Revised Union Version

9 Walakini hawakusikia; naye Manase akawakosesha wafanye mabaya, kuliko mataifa BWANA aliowaharibu mbele za wana wa Israeli.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Lakini hawakusikia, naye Manase aliwafanya watende dhambi zaidi kuliko zile zilizofanywa na mataifa ambayo Mwenyezi-Mungu aliyaharibu mbele ya Waisraeli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Lakini hawakusikia, naye Manase aliwafanya watende dhambi zaidi kuliko zile zilizofanywa na mataifa ambayo Mwenyezi-Mungu aliyaharibu mbele ya Waisraeli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Lakini hawakusikia, naye Manase aliwafanya watende dhambi zaidi kuliko zile zilizofanywa na mataifa ambayo Mwenyezi-Mungu aliyaharibu mbele ya Waisraeli.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Lakini hawa watu hawakusikiliza. Manase akawapotosha, kiasi kwamba walifanya maovu mengi kuliko mataifa ambayo Mwenyezi Mungu aliangamiza mbele ya Waisraeli.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Lakini hawa watu hawakusikiliza. Manase akawapotosha, hivyo kwamba walifanya maovu mengi kuliko mataifa ambayo bwana aliyaangamiza mbele ya Waisraeli.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

9 Walakini hawakusikia; naye Manase akawakosesha wafanye mabaya, kuliko mataifa BWANA aliowaharibu mbele za wana wa Israeli.

Tazama sura Nakili




2 Wafalme 21:9
25 Marejeleo ya Msalaba  

Naye atawatoa Israeli kwa ajili ya makosa ya Yeroboamu, aliyoyakosa, ambayo kwa hayo amewakosesha Israeli.


Lakini aliiendea njia ya wafalme wa Israeli, hata akampitisha mwanawe motoni, sawasawa na machukizo ya mataifa BWANA aliowafukuza mbele ya wana wa Israeli.


BWANA akanena kwa watumishi wake manabii, akisema,


Basi Manase aliwapotosha Yuda na wenyeji wa Yerusalemu, hata wakazidi kufanya mabaya kuliko mataifa, aliowaharibu BWANA mbele ya wana wa Israeli.


lakini waliwadhihaki wajumbe wa Mungu, na kuyadharau maneno yake, na kuwacheka manabii wake, hata ilipozidi ghadhabu ya BWANA juu ya watu wake, hata kusiwe na kuponya.


Walakini hawakukutii, wakakuasi, wakaitupa sheria yako nyuma yao, wakawaua manabii wako waliowaonya ili wapate kukurudia wewe; wakakufuru sana.


Wasio haki hutembea pande zote, Huku ufisadi ukitukuka kati ya wanadamu.


Mimi ndimi BWANA, Mungu wako, Niliyekupandisha toka nchi ya Misri; Fumbua sana kinywa chako nami nitakijaza.


Mwenye kutawala akisikiliza uongo; Basi watumishi wake wote watakuwa waovu.


nanyi mtajua ya kuwa mimi ni BWANA; kwa maana hamuendi katika amri zangu, wala hamkuzishika hukumu zangu, bali mmetenda mambo kama hukumu za mataifa wanaowazunguka.


Lakini hukuenda katika njia zao, na hukutenda kulingana na machukizo yao; lakini kwa kitambo kidogo ulikuwa umepotoka kuliko wao katika njia zako zote.


Nawe utasema, Bwana MUNGU asema hivi; Mji umwagao damu ndani yake, ili wakati wake upate kuja; mji ufanyao vinyago juu ya nafsi yake, ili ujitie unajisi!


Nao umeasi amri zangu, kwa kutenda mabaya kuliko mataifa hayo, nao umeasi sheria kuliko nchi hizo ziuzungukazo; maana wamezikataa hukumu zangu, wala hawakuenda katika sheria zangu.


Basi, kwa hiyo Bwana MUNGU asema hivi; Kwa sababu ninyi mmefanya ghasia kuliko mataifa wawazungukao ninyi, wala hamkuenda katika sheria zangu, wala hamkuzishika amri zangu, wala hamkutenda kama kawaida za mataifa wawazungukao;


wala hatukuwasikiliza watumishi wako, manabii, ambao kwa jina lako walisema na wafalme wetu, na wakuu wetu, na baba zetu, na watu wote wa nchi.


Efraimu ameonewa, amesetwa katika hukumu, kwa sababu alikuwa radhi kufuata ubatili.


Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii na kuwapiga kwa mawe waliotumwa kwako, mara ngapi nimetaka kuwakusanya watoto wako kama vile kuku awakusanyavyo vifaranga wake chini ya mbawa zake, wala hamkutaka.


Kama nisingalikuja na kusema nao, wasingalikuwa na dhambi; lakini sasa hawana kisingizio kwa dhambi yao.


Basi yeye ajuaye kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi.


Lakini nina neno juu yako, ya kwamba wamridhia yule mwanamke Yezebeli, yeye ajiitaye nabii na kuwafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, ili wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu.


Lakini hao watu wakakataa kuisikiliza sauti ya Samweli; wakasema, Sivyo hivyo; lakini tunataka kuwa na mfalme juu yetu;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo