Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




2 Wafalme 21:4 - Swahili Revised Union Version

4 Akazijenga madhabahu ndani ya nyumba ya BWANA, napo ndipo alipopanena BWANA, Katika Yerusalemu nitaliweka jina langu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Alijenga madhabahu katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu mahali ambapo Mwenyezi-Mungu alikuwa amesema, “Jina langu litaabudiwa katika Yerusalemu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Alijenga madhabahu katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu mahali ambapo Mwenyezi-Mungu alikuwa amesema, “Jina langu litaabudiwa katika Yerusalemu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Alijenga madhabahu katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu mahali ambapo Mwenyezi-Mungu alikuwa amesema, “Jina langu litaabudiwa katika Yerusalemu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Akajenga madhabahu katika Hekalu la Mwenyezi Mungu, ambamo Mwenyezi Mungu alikuwa amesema, “Katika Yerusalemu nitaliweka Jina langu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Akajenga madhabahu katika Hekalu la bwana, ambamo bwana alikuwa amesema, “Katika Yerusalemu nitaliweka Jina langu.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

4 Akazijenga madhabahu ndani ya nyumba ya BWANA, napo ndipo alipopanena BWANA, Katika Yerusalemu nitaliweka jina langu.

Tazama sura Nakili




2 Wafalme 21:4
18 Marejeleo ya Msalaba  

Yeye ndiye atakayejenga nyumba kwa jina langu, nacho kiti cha enzi cha ufalme wake nitakiimarisha milele.


Macho yako yafumbuke na kuielekea nyumba hii usiku na mchana, mahali hapa ulipopataja, ukasema, Hapa ndipo litakapokuwapo jina langu; ili uyasikie maombi ya mtumwa wako aombapo akikabili mahali hapa.


BWANA akamwambia, Nimeyasikia maombi yako na dua zako, ulizotoa mbele zangu. Nimeitakasa nyumba hii uliyoijenga ili niweke jina langu humo milele; tena macho yangu na moyo wangu utakuwapo hapo siku zote;


Nazo madhabahu zilizokuwako darini juu ya chumba cha juu cha Ahazi, wafalme wa Yuda walizozifanya, nazo madhabahu alizozifanya Manase katika behewa mbili za nyumba ya BWANA, mfalme akazivunja, akaziteremsha huko nje, na kuyatupa mavumbi yake katika kijito cha Kidroni.


BWANA akasema Nitawahamisha Yuda pia mbali nami, kama nilivyowahamisha Israeli, nami nitautupa mji huu niliouchagua, naam, Yerusalemu, na nyumba ile niliyoinena, Jina langu litakuwa humo.


Tangu siku ile nilipowatoa watu wangu katika nchi ya Misri, sikuchagua mji wowote wa kabila zote za Israeli ili kujenga nyumba, jina langu liwe humo; wala sikumchagua mtu yeyote awe mkuu juu ya watu wangu Israeli;


lakini nimeuchagua Yerusalemu, jina langu liwe humo; na Daudi nimemchagua awe juu ya watu wangu Israeli.


Utanifanyia madhabahu ya udongo, nawe utatoa dhabihu zako juu yake; sadaka za kuteketezwa, na sadaka za amani, kondoo wako, na ng'ombe wako, kila mahali nitakapotia ukumbusho wa jina langu, hapo ndipo nitakapokujilia na kukubarikia.


Kwa kuwa mji huu umekuwa sababu ya kunitia hasira, na sababu ya ghadhabu yangu, tangu siku ile walipoujenga hata siku hii ya leo; ili niuondoe usiwe mbele za uso wangu;


Bali waliweka machukizo yao ndani ya nyumba iliyoitwa kwa jina langu, ili kuinajisi.


Tena walijenga mahali palipoinuka kwa Baali, palipo katika bonde la mwana wa Hinomu, ili kuwapitisha wana wao na binti zao katika moto kwa ajili ya Moleki, jambo nisilowaagiza; wala halikuingia moyoni mwangu kwamba walitende chukizo hilo; wapate kumkosesha Yuda.


Maana wana wa Yuda wametenda yaliyo maovu machoni pangu, asema BWANA; wameweka machukizo yao ndani ya nyumba hiyo, iitwayo kwa jina langu, hata kuitia unajisi.


Tena wamenitenda haya; wamepatia unajisi mahali pangu patakatifu, siku ile ile, nao wamezitangua sabato zangu.


Kwa maana walipokuwa wamekwisha kuvichinjia vinyago vyao watoto wao, ndipo walipoingia patakatifu pangu, siku ile ile, wapatie unajisi, na tazama, wamefanya hivyo katika nyumba yangu.


Lakini mahali atakapochagua BWANA, Mungu wenu, katika makabila yenu yote, apaweke jina lake, maana, ni makao yake, elekezeni nyuso zenu hapo, nawe uende huko;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo