Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




2 Wafalme 21:2 - Swahili Revised Union Version

2 Akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA, sawasawa na machukizo ya mataifa, aliowafukuza BWANA mbele ya wana wa Israeli.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Alitenda maovu mbele ya Mwenyezi-Mungu kwa kuiga mienendo miovu ya mataifa ambayo yalifukuzwa na Mwenyezi-Mungu wakati watu wake, Waisraeli walipokuwa wanaingia nchini.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Alitenda maovu mbele ya Mwenyezi-Mungu kwa kuiga mienendo miovu ya mataifa ambayo yalifukuzwa na Mwenyezi-Mungu wakati watu wake, Waisraeli walipokuwa wanaingia nchini.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Alitenda maovu mbele ya Mwenyezi-Mungu kwa kuiga mienendo miovu ya mataifa ambayo yalifukuzwa na Mwenyezi-Mungu wakati watu wake, Waisraeli walipokuwa wanaingia nchini.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Akafanya maovu machoni pa Mwenyezi Mungu, akafuata desturi za machukizo za mataifa ambayo Mwenyezi Mungu aliyafukuza mbele ya Waisraeli.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Akafanya maovu machoni pa bwana, akafuata desturi za machukizo za mataifa ambayo bwana aliyafukuza mbele ya Waisraeli.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

2 Akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA, sawasawa na machukizo ya mataifa, aliowafukuza BWANA mbele ya wana wa Israeli.

Tazama sura Nakili




2 Wafalme 21:2
20 Marejeleo ya Msalaba  

Akafanya yaliyo maovu machoni pa BWANA, ila si kama wafalme wa Israeli waliomtangulia.


Kwa sababu Manase mfalme wa Yuda amefanya machukizo haya, na kutenda vibaya kuliko yote waliyoyatenda Waamori, waliokuwa kabla yake, naye akawakosesha Yuda kwa sanamu zake;


Na Manase akazimwaga damu zisizo na hatia, nyingi sana, hata alipokuwa ameijaza Yerusalemu tangu upande huu hata upande huu; zaidi ya kosa lake alilowakosesha Yuda, kutenda yaliyo mabaya machoni pa BWANA.


Akafanya yaliyo maovu machoni pa BWANA, kama Manase babaye alivyofanya.


Akaiendea njia yote aliyoiendea baba yake, akazitumikia sanamu alizozitumikia baba yake, akaziabudu.


Akaiweka sanamu ya kuchongwa ya Ashera aliyoifanya ndani ya nyumba, ambayo BWANA alimwambia Daudi, na Sulemani mwanawe, Katika nyumba hii, na katika Yerusalemu, niliouchagua miongoni mwa kabila zote za Israeli, nitaliweka jina langu milele;


kwa sababu wameniacha mimi, wameifukizia uvumba miungu mingine, ili wapate kunikasirisha kwa kazi yote ya mikono yao; kwa hiyo hasira yangu itawaka juu ya mahali hapa, isizimike.


Akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA, sawasawa na yote waliyoyafanya baba zake.


Akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA, mfano wa yote aliyoyafanya baba yake.


Na zaidi ya hayo wakuu wote wa makuhani, na watu, wakakosa mno wakifuata machukizo yote ya mataifa; wakainajisi nyumba ya BWANA aliyoitakasa katika Yerusalemu.


Hekima ndiyo bora kupita silaha za vita; Lakini mkosaji mmoja huharibu mema mengi.


Mimi nami nitachagua mapigo yao, nitaleta hofu zao juu yao; kwa sababu nilipoita, hawakuitika; na niliponena, hawakusikia; bali walifanya yaliyo maovu machoni pangu, na kuyachagua nisiyoyafurahia.


Nami nitawafanya kuwa kitu cha kutisha katika falme zote za duniani, kwa sababu ya Manase, mwana wa Hezekia mfalme wa Yuda, kwa sababu ya mambo aliyoyatenda katika Yerusalemu.


nanyi mtajua ya kuwa mimi ni BWANA; kwa maana hamuendi katika amri zangu, wala hamkuzishika hukumu zangu, bali mmetenda mambo kama hukumu za mataifa wanaowazunguka.


Samaria naye hakutenda nusu ya dhambi zako; bali wewe umeyaongeza machukizo yako zaidi ya hao, nawe umewapa haki dada zako kwa machukizo yako yote uliyoyatenda.


Nawe utasema, Bwana MUNGU asema hivi; Mji umwagao damu ndani yake, ili wakati wake upate kuja; mji ufanyao vinyago juu ya nafsi yake, ili ujitie unajisi!


Usimtende kama haya BWANA, Mungu wako; kwani kila yaliyo machukizo kwa BWANA, ayachukiayo yeye, wameifanyia miungu yao; kwa maana hata wana wao na binti zao huiteketezea hiyo miungu yao ndani ya moto.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo