Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




2 Wafalme 19:22 - Swahili Revised Union Version

22 Ni nani uliyemshutumu na kumtukana? Umeinua sauti yako juu ya nani, na kuinua macho yako juu? Juu ya Mtakatifu wa Israeli.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

22 Je, uliyekuwa unamkashifu na kumdhihaki ni nani? Nani umemwinulia sauti na kumkodolea macho kwa kiburi? Juu ya Mtakatifu wa Israeli!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

22 Je, uliyekuwa unamkashifu na kumdhihaki ni nani? Nani umemwinulia sauti na kumkodolea macho kwa kiburi? Juu ya Mtakatifu wa Israeli!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

22 Je, uliyekuwa unamkashifu na kumdhihaki ni nani? Nani umemwinulia sauti na kumkodolea macho kwa kiburi? Juu ya Mtakatifu wa Israeli!”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

22 Ni nani uliyemtukana na kumkufuru? Ni nani uliyepaza sauti yako dhidi yake, na kumwinulia macho yako kwa kiburi? Ni dhidi ya yule Aliye Mtakatifu wa Israeli!

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

22 Ni nani uliyemtukana na kumkufuru? Ni nani uliyeinua sauti yako dhidi yake, na kumwinulia macho yako kwa kiburi? Ni dhidi ya yule Aliye Mtakatifu wa Israeli!

Tazama sura Nakili




2 Wafalme 19:22
22 Marejeleo ya Msalaba  

Yamkini BWANA, Mungu wako, atayasikia maneno yote ya kamanda huyu, ambaye mfalme wa Ashuru, bwana wake, amemtuma ili amtukane Mungu aliye hai; naye atayakemea hayo maneno aliyoyasikia BWANA, Mungu wako; kwa sababu hii inua dua yako kwa ajili ya mabaki yaliyobakia.


Isaya akawaambia, Mwambieni bwana wenu maneno haya; BWANA asema hivi, Usiyaogope maneno hayo uliyoyasikia, ambayo watumishi wa mfalme wa Ashuru wamenitukana.


Nami nitakushukuru kwa kinanda, Na kweli yako, Ee Mungu wangu. Nitakuimbia Wewe kwa kinubi, Ee Mtakatifu wa Israeli.


Wameweka kinywa chao mbinguni, Na ulimi wao hutangatanga duniani.


Wakamjaribu Mungu tena na tena; Na kumkasirisha Mtakatifu wa Israeli.


Farao akasema, BWANA ni nani, hata niisikilize sauti yake, na kuwapa Israeli ruhusa waende zao? Mimi simjui BWANA, wala sitawapa Israeli ruhusa waende zao.


Nawe, je! Hata sasa wajitukuza juu ya watu wangu, usiwape ruhusa waende zao?


Kuna kizazi cha watu ambao macho yao yameinuka kama nini! Na kope zao zimeinuka sana.


Kwa maana amesema, Kwa nguvu za mkono wangu nimetenda jambo hili, na kwa hekima yangu; maana mimi nina busara; nami nimeiondoa mipaka ya watu, nikaziteka akiba zao, nikawaangusha waketio juu ya viti vya enzi kama afanyavyo shujaa.


Je! Shoka lijisifu juu yake alitumiaye? Je! Msumeno ujitukuze juu yake auvutaye? Ingekuwa kana kwamba bakora ingewatikisa waiinuao, au fimbo ingemwinua yeye ambaye si mti.


Kwa maana Bwana MUNGU, Mtakatifu wa Israeli, asema hivi, Kwa kurudi na kustarehe mtaokolewa; nguvu zenu zitakuwa katika kutulia na kutumaini; lakini hamkukubali.


Kwa hiyo kama vile muali wa moto uteketezavyo mabua makavu, na kama manyasi makavu yaangukavyo katika muali wa moto; kadhalika shina lao litakuwa kama ubovu, na ua lao litapeperushwa juu kama mavumbi; kwa sababu wameikataa sheria ya BWANA wa majeshi, na kulidharau neno lake aliye Mtakatifu wa Israeli.


Kwa maana Israeli, wala Yuda, hakuachwa na Mungu wake, BWANA wa majeshi; ijapokuwa nchi yao imejaa hatia juu yake aliye Mtakatifu wa Israeli.


Naam, ikajitukuza hata juu yake aliye mkuu wa jeshi hilo, ikamwondolea sadaka ya kuteketezwa ya daima, na mahali pa patakatifu pake pakaangushwa chini.


tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo;


yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama cha kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo