2 Wafalme 17:9 - Swahili Revised Union Version9 Tena, wana wa Israeli wakafanya kwa siri mambo yasiyokuwa mema juu ya BWANA, Mungu wao, wakajijengea mahali pa juu katika miji yao yote, kutoka mnara wa walinzi hata katika miji yenye boma. Tazama suraMatoleo zaidiBiblia Habari Njema9 Watu wa Israeli walitenda kwa siri mambo yasiyokuwa mema mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wao. Walijenga mahali pa juu pa kuabudia miungu ya uongo katika kila mji, kuanzia mnara wa walinzi mashambani hadi katika mji wenye ngome. Tazama suraBiblia Habari Njema - BHND9 Watu wa Israeli walitenda kwa siri mambo yasiyokuwa mema mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wao. Walijenga mahali pa juu pa kuabudia miungu ya uongo katika kila mji, kuanzia mnara wa walinzi mashambani hadi katika mji wenye ngome. Tazama suraBiblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza9 Watu wa Israeli walitenda kwa siri mambo yasiyokuwa mema mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wao. Walijenga mahali pa juu pa kuabudia miungu ya uongo katika kila mji, kuanzia mnara wa walinzi mashambani hadi katika mji wenye ngome. Tazama suraNeno: Bibilia Takatifu9 Waisraeli wakafanya vitu kwa siri dhidi ya Mwenyezi Mungu, Mungu wao, ambavyo havikuwa sawa. Kuanzia kwenye mnara wa ulinzi hadi kwenye mji wenye ngome, walijijengea mahali pa juu pa kuabudia miungu katika miji yao yote. Tazama suraNeno: Maandiko Matakatifu9 Waisraeli wakafanya vitu kwa siri dhidi ya bwana Mwenyezi Mungu wao, ambavyo havikuwa sawa. Kuanzia kwenye mnara wa ulinzi hadi kwenye mji wenye maboma walijijengea wenyewe mahali pa juu pa kuabudia miungu katika miji yao yote. Tazama suraBIBLIA KISWAHILI9 Tena, wana wa Israeli wakafanya kwa siri mambo yasiyokuwa mema juu ya BWANA, Mungu wao, wakajijengea mahali pa juu katika miji yao yote, kutoka mnara wa walinzi hata katika miji yenye boma. Tazama sura |
Kwa maana nilipokuwa nimekwisha kuwaingiza katika nchi ile, ambayo niliuinua mkono wangu kuwapa, wakati huo walipoona kila mlima mrefu, na kila mti wenye majani mengi, walitoa matoleo yao huko, na huko walitoa chukizo la sadaka zao, na huko walifukiza manukato ya kupendeza, na huko walimimina sadaka zao za kunywewa.