Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

2 Wafalme 13:25 - Swahili Revised Union Version

25 Naye Yehoashi, mwana wa Yehoahazi, akaitwaa tena mkononi mwa Ben-hadadi mwana wa Hazaeli miji ile aliyoitwaa yeye mkononi mwa Yehoahazi baba yake vitani. Mara tatu Yehoashi akamshinda, akairudisha miji ya Israeli.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

25 Mfalme Yehoashi alimshinda Ben-hadadi mara tatu na kuikomboa miji yote iliyotekwa wakati wa utawala wa Yehoahazi, baba yake Yehoashi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

25 Mfalme Yehoashi alimshinda Ben-hadadi mara tatu na kuikomboa miji yote iliyotekwa wakati wa utawala wa Yehoahazi, baba yake Yehoashi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

25 Mfalme Yehoashi alimshinda Ben-hadadi mara tatu na kuikomboa miji yote iliyotekwa wakati wa utawala wa Yehoahazi, baba yake Yehoashi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

25 Kisha Yehoashi mwana wa Yehoahazi akateka tena kutoka kwa Ben-Hadadi mwana wa Hazaeli ile miji aliyokuwa ameitwaa kwa vita kutoka kwa baba yake Yehoahazi. Yehoashi alimshinda mara tatu, hivyo akaweza kuiteka tena ile miji ya Waisraeli.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Wafalme 13:25
8 Marejeleo ya Msalaba  

Wakatua kuelekeana muda wa siku saba. Ikawa siku ya saba vikapangwa vita; wana wa Israeli wakawapiga miongoni mwa Washami siku moja watu laki moja waendao kwa miguu.

Siku zile BWANA akaanza kupunguza Israeli. Hazaeli akawapiga kote mipakani mwa Israeli;

kutoka Yordani upande wa mashariki, nchi yote ya Gileadi, na ya Wagadi, na Wareubeni, na Wamanase, kutoka Aroeri iliopo karibu na bonde la Arnoni, yaani, Gileadi, na Bashani.

Akafa Hazaeli mfalme wa Shamu, na Ben-hadadi mwanawe akatawala mahali pake.

Hasira ya BWANA ikawaka juu ya Israeli, akawatia mkononi mwa Hazaeli mfalme wa Shamu, na mkononi mwa Ben-hadadi mwana wa Hazaeli, siku zote.

(BWANA akawapa Israeli mwokozi, nao wakatoka mikononi mwa Washami; wana wa Israeli wakakaa hemani mwao kama zamani za kwanza.

Yeye akaurudisha mpaka wa Israeli toka kuingia kwa Hamathi hata bahari ya Araba, sawasawa na neno la BWANA, Mungu wa Israeli, alilolinena kwa mkono wa mtumishi wake Yona mwana wa Amitai, nabii, aliyekuwa wa Gath-heferi.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo