2 Wafalme 12:10 - Swahili Revised Union Version10 Ikawa, walipoona ya kuwa fedha nyingi imo kashani, karani wa mfalme akapanda na kuhani mkuu, wakaifunga mifukoni, wakaihesabu fedha iliyoonekana nyumbani mwa BWANA. Tazama suraMatoleo zaidiBiblia Habari Njema10 Kila walipoona kuwa mna fedha nyingi sandukuni, katibu wa mfalme na kuhani mkuu waliingia na kuhesabu na kuzifunga katika vifurushi fedha zote zilizopatikana katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Tazama suraBiblia Habari Njema - BHND10 Kila walipoona kuwa mna fedha nyingi sandukuni, katibu wa mfalme na kuhani mkuu waliingia na kuhesabu na kuzifunga katika vifurushi fedha zote zilizopatikana katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Tazama suraBiblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza10 Kila walipoona kuwa mna fedha nyingi sandukuni, katibu wa mfalme na kuhani mkuu waliingia na kuhesabu na kuzifunga katika vifurushi fedha zote zilizopatikana katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Tazama suraNeno: Bibilia Takatifu10 Kila mara walipoona kuwa kuna kiasi kikubwa cha fedha ndani ya kisanduku, mwandishi wa mfalme na kuhani mkuu walikuja, wakazihesabu fedha hizo zilizoletwa katika Hekalu la Mwenyezi Mungu, na kuziweka katika mifuko. Tazama suraNeno: Maandiko Matakatifu10 Kila mara walipoona kuwa kuna kiasi kikubwa cha fedha ndani ya kisanduku, mwandishi wa mfalme na kuhani mkuu walikuja, wakazihesabu fedha hizo zilizoletwa katika Hekalu la bwana, na kuziweka katika mifuko. Tazama suraBIBLIA KISWAHILI10 Ikawa, walipoona ya kuwa fedha nyingi imo kashani, karani wa mfalme akapanda na kuhani mkuu, wakaifunga mifukoni, wakaihesabu fedha iliyoonekana nyumbani mwa BWANA. Tazama sura |
Kisha, mfalme akamwamuru Hilkia, kuhani mkuu, na makuhani wa daraja ya pili, na walinzi wa mlango, kwamba watoe katika hekalu la BWANA vyombo vyote vilivyofanywa kwa ajili ya Baali, na kwa ajili ya Ashera, na kwa ajili ya jeshi lote la mbinguni; akaviteketeza kwa moto nje ya Yerusalemu, katika mashamba ya Ridroni, akayachukua majivu yake mpaka Betheli.
Ikawa wakati walipoletewa kasha wasimamizi wa mfalme kwa mkono wa Walawi, nao wakaona ya kwamba kuna fedha nyingi, huja karani wa mfalme, na msimamizi wake kuhani mkuu, wakatoa yaliyomo kashani, kisha hulichukua kasha, na kulirudisha mahali pake. Ndivyo walivyofanya siku kwa siku, wakakusanya fedha tele.