Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




2 Wafalme 11:19 - Swahili Revised Union Version

19 Akawatwaa wakuu wa mamia, na Wakari, na walinzi, na watu wote wa nchi; wakamleta mfalme kushuka nyumbani mwa BWANA, wakaja kwa njia ya mlango wa walinzi mpaka nyumba ya mfalme. Naye akakaa katika kiti cha enzi cha wafalme.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Aliwachukua makapteni, Wakari na wakazi wote; nao wakamsindikiza mfalme kutoka nyumba ya Mwenyezi-Mungu wakapitia katika lango la walinzi mpaka ikulu. Naye akakikalia kiti cha enzi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Aliwachukua makapteni, Wakari na wakazi wote; nao wakamsindikiza mfalme kutoka nyumba ya Mwenyezi-Mungu wakapitia katika lango la walinzi mpaka ikulu. Naye akakikalia kiti cha enzi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Aliwachukua makapteni, Wakari na wakazi wote; nao wakamsindikiza mfalme kutoka nyumba ya Mwenyezi-Mungu wakapitia katika lango la walinzi mpaka ikulu. Naye akakikalia kiti cha enzi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Pamoja naye akawachukua majemadari wa mamia, Wakari, walinzi na watu wote wa nchi, nao kwa pamoja wakamteremsha mfalme kutoka Hekalu la Mwenyezi Mungu na kwenda kwenye jumba la mfalme, wakiingilia njia ya lango la walinzi. Ndipo mfalme akachukua nafasi yake kwenye kiti cha ufalme;

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Pamoja naye akawachukua majemadari wa mamia, Wakari, walinzi na watu wote wa nchi, nao kwa pamoja wakamteremsha mfalme kutoka Hekalu la bwana na kwenda kwenye jumba la mfalme, wakiingilia njia ya lango la walinzi. Ndipo mfalme akachukua nafasi yake kwenye kiti cha enzi,

Tazama sura Nakili




2 Wafalme 11:19
13 Marejeleo ya Msalaba  

Nao Wamidiani wakamuuza huko Misri, kwa Potifa, mmoja wa maofisa wa Farao, mkuu wa askari walinzi.


Nenda uingie ndani kwa mfalme Daudi, ukamwambie, Je! Hukuniapia mimi mjakazi wako, Ee mfalme, bwana wangu, kusema, Hakika yake Sulemani mwana wako atamiliki baada yangu, na kuketi katika kiti changu cha enzi? Mbona basi anamiliki Adonia?


Mfalme Rehoboamu akatengeneza ngao za shaba mahali pake, akawakabidhi wakuu wa walinzi, waliongoja mlangoni pa nyumba ya mfalme.


Ndipo Sulemani akaketi katika kiti cha enzi cha BWANA, awe mfalme badala ya Daudi babaye, akafanikiwa; nao Israeli wote wakamtii.


Akawaweka walinzi malangoni pa nyumba ya BWANA, asiingie aliye najisi kwa namna yoyote.


Akawatwaa makamanda wa mamia, na watu wakubwa, na hao watawalao watu, na watu wote wa nchi, akamteremsha mfalme kutoka nyumba ya BWANA; wakalipitia lango la juu waende nyumbani kwa mfalme, wakamketisha mfalme katika kiti cha ufalme.


na theluthi nyumbani pa mfalme; na theluthi langoni pa msingi; na watu wote watakuwapo nyuani mwa nyumba ya BWANA.


ndipo watakapoingia wafalme na wakuu kwa malango ya mji huu; wataketi katika kiti cha enzi cha Daudi, na kupanda magari na farasi, wao, na wakuu wao, watu wa Yuda, na wenyeji wa Yerusalemu; na mji huu utakaa hata milele.


BWANA asema hivi, Andikeni habari za mtu huyu kwamba hana watoto, kwamba mtu huyu hatafanikiwa siku zake zote; maana hapana mtu katika wazao wake atakayefanikiwa, akiketi katika kiti cha enzi cha Daudi, na kutawala tena katika Yuda.


Kwa maana mkifanya haya kweli kweli, ndipo watakapoingia kwa malango ya nyumba hii wafalme wenye kuketi katika kiti cha enzi cha Daudi, wanakwenda kwa magari, na wamepanda farasi, yeye, na watumishi wake, na watu wake.


Yesu akawaambia, Amin, nawaambia ya kwamba ninyi mlionifuata mimi, katika ulimwengu mpya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti kumi na viwili, mkiwahukumu makabila kumi na mawili ya Israeli.


Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo