Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

2 Wafalme 10:10 - Swahili Revised Union Version

10 Jueni basi ya kwamba halianguki chini lolote la neno la BWANA, alilolinena BWANA juu ya nyumba ya Ahabu; kwa maana BWANA ameyafanya hayo aliyoyanena kwa kinywa cha mtumishi wake Eliya.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Jueni ya kwamba maneno yote aliyosema Mwenyezi-Mungu kuhusu jamaa ya Ahabu yametimia. Mwenyezi-Mungu ameyafanya hayo aliyosema kwa njia ya mtumishi wake Elia.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Jueni ya kwamba maneno yote aliyosema Mwenyezi-Mungu kuhusu jamaa ya Ahabu yametimia. Mwenyezi-Mungu ameyafanya hayo aliyosema kwa njia ya mtumishi wake Elia.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Jueni ya kwamba maneno yote aliyosema Mwenyezi-Mungu kuhusu jamaa ya Ahabu yametimia. Mwenyezi-Mungu ameyafanya hayo aliyosema kwa njia ya mtumishi wake Elia.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Fahamuni basi kwamba, hakuna neno ambalo Mwenyezi Mungu amesema dhidi ya nyumba ya Ahabu ambalo halitatimia. Mwenyezi Mungu amefanya lile aliloahidi kupitia mtumishi wake Ilya.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Fahamuni basi kwamba, hakuna neno ambalo bwana amesema dhidi ya nyumba ya Ahabu ambalo halitatimia. bwana amefanya lile aliloahidi kupitia mtumishi wake Ilya.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

10 Jueni basi ya kwamba halianguki chini lolote la neno la BWANA, alilolinena BWANA juu ya nyumba ya Ahabu; kwa maana BWANA ameyafanya hayo aliyoyanena kwa kinywa cha mtumishi wake Eliya.

Tazama sura Nakili

2 Wafalme 10:10
13 Marejeleo ya Msalaba  

Ukamwambie, ukisema, BWANA asema hivi, Je! Umeua, ukatamalaki? Nawe utamwambia, kusema, BWANA asema hivi, Mahali pale mbwa walipoiramba damu ya Nabothi, mbwa watairamba na damu yako, naam, damu yako.

Huoni jinsi Ahabu alivyojidhili mbele yangu? Basi kwa sababu amejidhili mbele yangu, sitayaleta yale mabaya katika siku zake; ila katika siku za mwanawe nitayaleta mabaya hayo juu ya nyumba yake.

Naye alipofika Samaria, aliwaua wote wa Ahabu waliokuwa wamebakia katika Samaria, hata akamwangamiza, sawasawa na neno la BWANA alilomwambia Eliya.

Hilo ndilo neno la BWANA alilomwambia Yehu, akisema, Wana wako watakaa kitini mwa Israeli hata kizazi cha nne. Ikawa vivyo hivyo.

Basi wakarudi, wakampasha habari. Akasema, Hili ndilo neno la BWANA, alilolinena kwa kinywa cha mtumishi wake Eliya, Mtishbi, kusema, Katika kiwanja cha Yezreeli mbwa wataila nyama ya Yezebeli.

Basi mfalme akamwambia Hamani, Hima! Twaa mavazi na farasi kama ulivyosema, ukamfanyie vivyo hivyo Mordekai, Myahudi, aketiye mlangoni pa mfalme; lisipungue neno lolote katika yote uliyoyasema.

Lakini maneno yangu, na amri zangu nilizowaagiza hao manabii, watumishi wangu, je, Hazikuwapata baba zenu? Nao wakatubu na kusema, BWANA wa majeshi ametutenda kulingana na njia zetu, na matendo yetu, kama alivyokusudia kutenda.

Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe.

Tena Yeye aliye Nguvu za Israeli hatanena uongo, wala hataona majuto; maana siye mwanadamu, hata ajute.

Samweli akakua, naye BWANA alikuwa pamoja naye, wala hakuliacha neno lake lolote lianguke chini.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo