Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




2 Samueli 24:12 - Swahili Revised Union Version

12 Nenda, ukanene na Daudi, BWANA asema hivi, Nakuwekea mambo matatu; katika haya uchague moja, nikutendee hilo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 “Nenda ukamwambie hivi Daudi: ‘Mwenyezi-Mungu asema hivi: Ninakupa mambo matatu, nawe ujichagulie mojawapo, nami nitakutendea.’”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 “Nenda ukamwambie hivi Daudi: ‘Mwenyezi-Mungu asema hivi: Ninakupa mambo matatu, nawe ujichagulie mojawapo, nami nitakutendea.’”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 “Nenda ukamwambie hivi Daudi: ‘Mwenyezi-Mungu asema hivi: Ninakupa mambo matatu, nawe ujichagulie mojawapo, nami nitakutendea.’”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 “Nenda ukamwambie Daudi, ‘Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu: Ninakupa wewe uchaguzi wa mambo matatu. Nichagulie mojawapo nitakalotenda dhidi yako.’ ”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 “Nenda ukamwambie Daudi, ‘Hivi ndivyo asemavyo bwana: Ninakupa wewe uchaguzi wa mambo matatu. Nichagulie mojawapo nitakalotenda dhidi yako.’ ”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

12 Nenda, ukanene na Daudi, BWANA asema hivi, Nakuwekea mambo matatu; katika haya uchague moja, nikutendee hilo.

Tazama sura Nakili




2 Samueli 24:12
13 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini, kwa kuwa kwa tendo hili umewapa adui za BWANA nafasi kubwa ya kukufuru, mtoto atakayezaliwa kwako hakika atakufa.


Na Daudi alipoondoka asubuhi, neno la BWANA likamjia nabii Gadi, mwonaji wake Daudi, na kusema,


Basi Gadi akamwendea Daudi, akamweleza, akamwambia, Basi, miaka saba ya njaa ikujie katika nchi yako? Au miezi mitatu ukimbie mbele ya adui zako, huku wakikufuatia? Au siku tatu iwe tauni katika nchi yako? Amua sasa, ufikiri, ni jawabu gani nimrudishie yeye aliyenituma.


Yoabu, mwana wa Seruya, alianza kuwahesabu, lakini hakumaliza; na ghadhabu ikawapata Israeli kwa hayo; wala hesabu hiyo haikuingizwa katika kumbukumbu za mfalme Daudi.


Kwa kuwa BWANA ampendaye humrudi, Kama vile baba mwanawe ampendezaye.


Maana mimi ni pamoja nawe, asema BWANA, nikuokoe; maana nitawakomesha kabisa mataifa yote huko nilikokutawanya, bali sitakukomesha wewe kabisa; lakini nitakurudi kwa hukumu, wala sitakuacha bila adhabu.


mimi nami nimewaendea kinyume, na kuwatia katika nchi ya adui zao; lakini hapo, kama mioyo yao isiyokuwa tohara ikinyenyekea, nao wakubali adhabu ya uovu wao;


Nchi nayo itaachwa na wao, nayo itazifurahia Sabato zake, itakapokuwa ukiwa pasipokuwa na wao; nao wataikubali adhabu ya uovu wao; kwa sababu wameyakataa maagizo yangu, na roho zao zimezichukia amri zangu.


Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo