Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

2 Samueli 18:28 - Swahili Revised Union Version

28 Ahimaasi akainua sauti yake, akamwambia mfalme, Amani. Akainama mbele ya mfalme kifudifudi, akasema, Ahimidiwe BWANA, Mungu wako, aliyewatoa watu hao walioiinua mikono yao juu ya bwana wangu, mfalme.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

28 Ndipo Ahimaasi akamwambia mfalme kwa sauti kubwa, “Mambo yote ni sawa.” Akainama mbele ya mfalme, akasujudu na kusema, “Na atukuzwe Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, ambaye amekukomboa kutoka watu walioinua mikono yao dhidi yako, bwana wangu mfalme.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

28 Ndipo Ahimaasi akamwambia mfalme kwa sauti kubwa, “Mambo yote ni sawa.” Akainama mbele ya mfalme, akasujudu na kusema, “Na atukuzwe Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, ambaye amekukomboa kutoka watu walioinua mikono yao dhidi yako, bwana wangu mfalme.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

28 Ndipo Ahimaasi akamwita mfalme, akasema, “Mambo yote ni mema!” Akasujudu mbele ya mfalme, uso wake ukigusa chini, akasema, “Ahimidiwe Mwenyezi Mungu, Mungu wako! Yeye aliyewatoa watu wale walioinua mikono yao dhidi ya mfalme bwana wangu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

28 Ndipo Ahimaasi akamwita mfalme, akasema, “Mambo yote ni mema!” Akasujudu mbele ya mfalme uso wake mpaka ardhini, akasema, “Ahimidiwe bwana Mwenyezi Mungu wako! Yeye aliyewatoa watu wale walioinua mikono yao dhidi ya mfalme bwana wangu.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

28 Ahimaasi akainua sauti yake, akamwambia mfalme, Amani. Akainama mbele ya mfalme kifudifudi, akasema, Ahimidiwe BWANA, Mungu wako, aliyewatoa watu hao walioiinua mikono yao juu ya bwana wangu, mfalme.

Tazama sura Nakili

2 Samueli 18:28
16 Marejeleo ya Msalaba  

Ahimidiwe Mungu Aliye Juu Sana, aliyewatia adui zako mikononi mwako. Abramu akampa fungu la kumi la vitu vyote.

Akasema, Na atukuzwe BWANA, Mungu wa bwana wangu Abrahamu, ambaye hakuacha rehema zake na kweli yake kwa bwana wangu. BWANA akaniongoza mimi nami njiani hata nyumba ya nduguze bwana wangu.

hata siku ya tatu ikawa, tazama! Akaja mtu kutoka kambi ya Sauli, nguo zake zimeraruliwa, tena ana mavumbi kichwani mwake; basi, ikawa alipomfikia Daudi, akaanguka chini, akamsujudia.

Naye yule mwanamke wa Tekoa aliponena na mfalme, akaanguka kifudifudi chini, akamsujudia, akasema, Nisaidie, Ee mfalme.

Kwake ajitakasaye utajionesha kuwa mtakatifu; Na kwa mpotovu utajionesha kuwa mkaidi.

Hata siku ya nne wakakusanyika katika bonde la Baraka; maana ndipo walipomtukuza BWANA; kwa hiyo jina lake mahali pale pakaitwa Bonde la Baraka hata leo.

Ee BWANA, kutukuza usitutukuze sisi, Bali ulitukuze jina lako, Kwa ajili ya fadhili zako, Kwa ajili ya uaminifu wako.

Na ahimidiwe BWANA; Asiyetutoa kuwa mawindo kwa meno yao.

Wala hukunitia mikononi mwa adui; Miguu yangu umeisimamisha mahali penye usalama.

Kisha Yethro akasema, Na ahimidiwe BWANA aliyewaokoa na mikono ya Wamisri, na mkono wa Farao; aliyewaokoa watu hao watoke mikononi mwa Wamisri.

Siku hii ya leo BWANA atakuua mkononi mwangu, nami nitakupiga, na kukuondolea kichwa chako, nami leo nitawapa ndege wa angani na wanyama wa nchi mizoga ya majeshi ya Wafilisti, ili kwamba dunia nzima wajue ya kuwa yuko Mungu katika Israeli.

Nawe umeonesha leo jinsi ulivyonitendea mema, kwani BWANA aliponitia mikononi mwako, hukuniua.

Ndipo hapo Abigaili alipomwona Daudi, alifanya haraka kushuka juu ya punda wake, akamwangukia Daudi kifudifudi, akainama mpaka chini.

Ndipo Abishai akamwambia Daudi, Mungu amemtia adui yako mikononi mwako leo; basi, niache nimpige kwa hilo fumo hadi chini kwa pigo moja, sitampiga mara ya pili.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo