Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




1 Yohana 5:7 - Swahili Revised Union Version

7 Naye Roho ndiye ashuhudiaye, kwa sababu Roho ndiye kweli.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Basi, wako mashahidi watatu:

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Basi, wako mashahidi watatu:

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Basi, wako mashahidi watatu:

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Kwa maana wako watatu washuhudiao [mbinguni: hao ni Baba, Neno na Roho wa Mungu. Hawa watatu ni umoja.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Kwa maana wako watatu washuhudiao[ mbinguni: hao ni Baba, Neno na Roho wa Mwenyezi Mungu. Hawa watatu ni umoja.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

7 Naye Roho ndiye ashuhudiaye, kwa sababu Roho ndiye kweli.

Tazama sura Nakili




1 Yohana 5:7
31 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa neno la BWANA mbingu ziliumbwa, Na jeshi lake lote kwa pumzi ya kinywa chake.


Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu BWANA amenitia mafuta niwahubirie wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwatibu waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao.


Alipokuwa bado akisema, tazama, wingu jeupe likawatia uvuli; na tazama, sauti ikatoka katika lile wingu, ikasema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye; msikieni yeye.


La, kama hasikii, chukua pamoja nawe tena mtu mmoja au wawili, ili kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno lithibitike.


Basi, nendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;


Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.


Mimi na Baba tu mmoja.


Baba, ulitukuze jina lako. Basi ikaja sauti kutoka mbinguni, Nimelitukuza, nami nitalitukuza tena.


ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.


Lakini ajapo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia.


Maana kama vile Baba alivyo na uzima nafsini mwake, vivyo hivyo alimpa na Mwana kuwa na uzima nafsini mwake.


Mimi ndimi ninayejishuhudia mwenyewe, naye Baba aliyenituma ananishuhudia.


Yesu akajibu, Nikijitukuza mwenyewe, utukufu wangu si kitu; anitukuzaye ni Baba yangu, ambaye ninyi mwanena kuwa ni Mungu wenu.


Basi yeye, akiisha kupandishwa hadi mkono wa kulia wa Mungu, na kupokea kwa Baba ile ahadi ya Roho Mtakatifu, amekimwaga kitu hiki mnachokiona sasa na kukisikia.


Na sisi tu mashahidi wa mambo haya, pamoja na Roho Mtakatifu ambaye Mungu amewapa wote wanaomtii.


Sikiliza, Ee Israeli; BWANA, Mungu wetu, BWANA ndiye mmoja


Lile lililokuwako tangu mwanzo, tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na mikono yetu ikalipapasa, kuhusu Neno la uzima;


Huyu ndiye aliyekuja kwa maji na damu, Yesu Kristo; si katika maji tu, bali katika maji na katika damu.


Kwa maana wako watatu washuhudiao [mbinguni, Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni umoja.


Naye amevikwa vazi lililoloweshwa katika damu, na jina lake anaitwa, Neno la Mungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo